Israel Jumatatu imeanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran, na kuibua vitisho vipya kutoka Iran hivyo kuongeza mgogoro ambao hivi sasa unasababisha mgogoro mkubwa wa nishati ambao haujawahi kutokea kwa miongo kadhaa.
Milipuko imesikika mjini Tehran, huku Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ukisema umedungua makombora mawili yaliyokuwa yanakuja na ndege zisizo na rubani huku mgogoro ukienea katika kanda.
Kwa mujibu wa Fatih Birol, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA), takriban maeneo 40 ya nishati katika nchi zinazotoa mafuta "yameharibiwa au yameharibiwa vibaya," huku vita vikiingia wiki yake ya nne.
Iran imejibu kwa mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kwa kulenga Israel, na maeneo ya nishati ya Ghuba pamoja na maeneo ya kidiplomasia ya Marekani, huku ikizuia upitaji wa meli katika Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu kwa upitishaji wa mamilioni ya mapipa ya mafuta kwa siku.
Kuongezeka kwa vitisho
Huku bei ya mafuta ikipanda na kufikia zaidi ya Dola za Marekani 100 kwa pipa, Donald Trump alitoa ilani, na kuionya Iran kuifungua Hormuz ndani ya saa 48 au iharibiwe miundombinu yake ya nishati.
Iran imejibu kwa hasira. Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf ametahadharisha kwamba miundombinu muhimu katika eneo hilo itakuwa ni "itakuwa ni halali yao kushambuliwa" iwapo Marekani itafanya inachotishia.
Birol amesema mgogoro huo tayari umeondoa mapipa ya mafuta ghafi milioni 11 katika mzunguko wa soko la dunia, ikizidi hasara iliyoonekana miaka ya 70.
“Hakuna nchi ambayo haitaathirika,” alionya, akitaka dunia kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo.














