UTURUKI
3 dk kusoma
Hamas inafuata makubaliano ya kusitisha mapigano, Israel inaendelea kuyakiuka, amesema Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amezungumzia kuhusu kujengwa upya kwa Gaza na viongozi wa Ghuba, akisema kuwa Kuwait, Qatar, na Oman wameonyesha dhamira thabiti ya kusaidia juhudi hizo .
Hamas inafuata makubaliano ya kusitisha mapigano, Israel inaendelea kuyakiuka, amesema Erdogan
Matamshi ya Rais Erdogan yanakuja wakati Uturuki inatafuta kuwa na nafasi kubwa katika juhudi za kimataifa za kuleta utulivu Gaza. / / AA
tokea masaa 12

Erdogan alisema kuwa mazungumzo yanaendelea kuhusiana na kuunda kikosi kazi cha kimataifa kitakachoendesha Gaza, na kwamba maelezo zaidi bado yanakamilishwa.

“Ni jambo lenye vipengele vingi, kwa hivyo mazungumzo ya kina yanaendelea,” Erdogan alisema kwa waandishi wa habari alipokuwa kwenye ndege yake Ijumaa, akirejea kutoka ziara zake Kuwait, Qatar na Oman. “Tuko tayari kutoa kila aina ya msaada, na maandalizi yetu yanaendelea.”

Kauli yake inakuja huku Uturuki ikisisitiza juhudi za kimataifa za kudumisha utulivu Gaza na kuhakikisha usitishaji vita uliyo dhaifu yanadumu, huku Israel ikiendelea kuyakiuka.

“Hamas inafuata makubaliano ya kusitisha mapiganoa na imethibitisha kwa uwazi dhamira yake ya kufanya hivyo,” Erdogan ameisema. “Israel, hata hivyo, inaendelea kuyakiuka. Jumuiya ya kimataifa, hasa Marekani, lazima iweke juhudi zaidi kuhakikisha Israel inatii kikamilifu.”

Erdogan alisema kuwa shinikizo la kidiplomasia kwa Israel ni “jambo muhimu,” na kuongeza kuwa vikwazo na kusitisha mauzo ya silaha vinaweza kusaidia kulazimisha Israel kutimiza ahadi zake.

InayohusianaTRT Afrika - Ziara ya Erdogan Ghuba: Uturuki, Qatar zasaini mikataba ya ulinzi na ushirikiano wa kimkakati

Juhudi za Uturuki za misaada wa kibinadamu na kujengwa upya kwa Gaza  

Erdogan ameahidi kuwa Uturuki itaendelea kutoa misaada ya kibinadamu isiyozuiliwa Gaza na kuchukua nafasi muhimu katika ujenzi upya wa eneo hilo lililoharibiwa na vita.

“Gaza itainuka tena — hakuna anayepaswa kutilia shaka hilo,” alisema. “Hatujawahi kuacha kutuma msaada wetu nchini Misri, na tutaendelea kufanya hivyo.”

Alibainisha kuwa Meli ya Wema ya 17 ya Uturuki, iliyobeba misaada ya kibinadamu, hivi karibuni ilifika Bandari ya El-Arish nchini Misri. Mashirika ya serikali ya Uturuki na isiyo ya serikali a, yamejipanga kusaidia kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa Gaza, amesema Erdogan.

“Ndugu zetu wa Gaza wanahitaji kila kitu kutokana na vikwazo vya kinyama vilivyowekwa na Israel,” Erdogan alisema. “Sasa ni wakati wa kuchukua hatua, si maneno.”

InayohusianaTRT Afrika - Erdogan akamilisha ziara ya Ghuba, akitia saini mikataba 24 mipya na Kuwait, Qatar na Oman

Uratibu wa kikanda kwa ajili ya kujenga upya Gaza

Erdogan alisema amejadili ujenzi upya wa Gaza na viongozi wa Ghuba wakati wa ziara yake ya kikanda, akiongeza kuwa Kuwait, Qatar na Oman zote zimeonyesha “dhamira thabiti na ya dhati” kusaidia juhudi hizo.

“Tutaijenga Gaza pamoja,” alisema. “Hili si jambo amnalo Uturuki, Misri, au nchi yoyote ya Ghuba wanaweza kufanya peke yao — ni juhudi ya watu wote.”

Aliipongeza Qatar kwa msaada wake wa muda mrefu kwa Palestina, akisema Gaza ni “mtihani kwa nchi za Kiislamu,” na akasema kuwa mawaziri wa Uturuki wanaendelea kuratibu na wenzao wa kikanda.

Uturuki iko tayari kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani Ukraine

Kuhusu vita vya Ukraine, Erdogan alisisitiza kuwa Uturuki iko tayari kuwa mwenyeji wa mazungumzo mapya ya amani kati ya Moscow na Kiev, baada ya ripoti kwamba mkutano wa Marekani–Urusi uliopangwa Budapest umekwama.

“Hii inaonyesha tena umuhimu wa maono ya amani ya Uturuki,” alisema.

“Tuna uhusiano mzuri na pande zote mbili na tumepata imani yao. Hii inatupa nafasi nzuri ya kutafuta amani, na tumeazimia kutumia nafasi hii kwa manufaa ya ubinadamu.”

CHANZO:TRT World