Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukika
AFRIKA
4 dk kusoma
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukikaUlimwenguni kote, kichaa cha mbwa huua takriban watu 59,000 kila mwaka, na karibu 95% ya vifo hivi hutokea Afrika na Asia.
Kwa wanadamu, huduma ya haraka ya jeraha na chanjo inaweza kuleta tofauti kati ya maisha na kifo. Picha/ GAVI - Pius Sawa
12 Novemba 2025

Mapema mwezi Oktoba, habari za kushtua zilitokeza kutoka New Delhi India. Kocha wa Kenya wa mashindano ya mbio Dennis Nzomo Ang'atwa na Mbwa katika Mashindano ya Dunia kwa walemavu yaliyokuwa yakiendelea huko.

Maelfu waliingia mtandaoni kuelezea kushtushwa na tukio hilo, mbali na hofu ya kuathiri utendaji wa timu ya Kenya, wengi walionesha hofu kwa afya ya Dennis.

Kung’atwa na mbwa kunaleta hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa.

‘‘Kutajwa tu kwa Kichaa cha Mbwa kunaleta hofu kubwa,’’ anasema daktari Traore Tiebe, afisa wa kiufundi wa afya na magonjwa ya wanyama pori katika WHO. ‘‘ Licha ya kuwa ni mojawapo ya magonjwa ya kale zaidi yanayojulikana, bado ni muuaji wa kimya kimya katika sehemu fulani za Afrika, na kuua maelfu ya maisha kila mwaka ila vifo hivyo inaweza kuzuilika,’’ anasema daktari Traore.

Hofu ya maambukizi

‘‘Wakati tulikuwa tunafanya mazoezi, niliinama kidogo nikimgongea mwenzangu kibao aanze mbio, nikasikia kitu kimenifinya mguuni, ‘‘ anasimiulia Dennis Nzomo katika video mtandaoni. ‘‘Mwanzo nilifikiria ni mtu amenifinya lakini kugeuka nikapata ni mbwa.’’ anaendelea kusimulia.

Nzomo kama mtu mwengine yeyote alihofia kuambukizwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa. alikimbili ahospitalini kutafuta usaidizi.

‘‘Nimeenda hospitali na siko vibaya sasa hivi. Nimedungwa mashindano kadhaa ya kinga ikiwemo ya pepo punda na ya kichaa cha mbwa,’’ anaelezea Nzomo

"Kichaa cha mbwa ni ugonjwa hatari unaoweza kuzuiwa unaoambukizwa na virusi vya wanyama pori vya familia ya Rhabdoviridae," aeleza Daktari Traore. "Husambazwa kwa wanadamu kupitia kugusana - haswa kuumwa na mikwaruzo - na wanyama wa nyumbani au wa porini walioambukizwa."

Maambukizi mengi hayaripotiwi

Ingawa ugonjwa wa kichaa cha mbwa hupatikana katika kila bara, umeenea zaidi katika nchi nyingi za Afrika. Virusi huendelea kuzunguka kwa kiasi kikubwa kupitia mbwa wa nyumbani, ambao ndio wahusika kwa hadi 99% ya maambukizi ya binadamu.

Kiwango cha kweli cha kichaa cha mbwa katika nchi za Afrika ni vigumu kujua. visa vingi haziripotiwi, haswa katika jamii za vijijini ambapo ufikiaji wa vituo vya afya na zana za uchunguzi ni mdogo.

"Kwa sababu maambukizi ya kichaa cha mbwa mara nyingi hayaripotiwi au kutambuliwa kimakosa, hatuna data kamili juu ya ni watu wangapi walioathiriwa au ni wanyama wangapi wanaobeba virusi," Daktari Traore anabainisha.

Ulimwenguni kote, kichaa cha mbwa huua takriban watu 59,000 kila mwaka, na karibu 95% ya vifo hivi hutokea Afrika na Asia. Ugonjwa huu huathiri zaidi maskini, ambao mara nyingi hawawezi kumudu au kupata matibabu ya PEP, chanjo ambayo inaweza kuzuia maambukizi baada ya kuumwa.

Watoto ndio walio hatarini zaidi.

"Asilimia 40 ya watu wanaoumwa na wanyama wanaoshukiwa kuwa na kichaa ni watoto walio chini ya umri wa miaka 15," Daktari Traore asema. "Tabia ya udadisi wao wa asili na tabia ya kucheza na wanyama huwaweka katika hatari kubwa."

Virusi vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa hujipenyeza ndani ya mwili kwa kuumwa au mkwaruzo na kusafiri kimya kwenye neva hadi kwenye ubongo. Mara tu inapofika kwenye ubongo, husababisha kuvimba ambayo husababisha kuchanganyikiwa, hofu ya maji kukusanya kwenye ubongo, kupooza - na hatimaye kifo.

"Baada ya dalili kuonekana, ugonjwa huo karibu kila wakati ni mbaya," Daktari Traore anaonya.

Kuna aina mbili kuu za kichaa cha mbwa kwa wanadamu. ‘Furious rabies’ , ambayo ndio ya kawaida zaidi, husababisha hasira, kuchanganyikiwa , na hofu ya maji. Nyingine ni ‘Paralytic rabies’ ambayo husambaa polepole, kuanzia na kodhoofisha misuli kabla ya kusababisha kukosa fahamu na kifo. Kwa sababu inaiga dalili zingine za mfumo wa neva, uchunguzi wa aina hii ya kichaa cha mbwa mara nyingi hutambuliwa vibaya - na kuchangia zaidi katika kukosa kuripotiwa.

Kuua mbwa koko mitaani sio suluhisho

Habari njema ni kwamba kichaa cha mbwa kinaweza kuzuilika kwa asili mia 100 - kwa wanyama na wanadamu.

Hatua bora zaidi ya kuzuia ni chanjo ya mbwa kwa wingi.

"Kuchanja mbwa, ikiwa ni pamoja na watoto wa mbwa, ndiyo njia bora zaidi ya kuzuia kichaa cha mbwa kwa watu. Inazuia virusi kwenye chanzo chake. Kuua mbwakoko mitaani sio suluhisho la ufanisi," Daktari Traore anasisitiza.

Kwa wanadamu, huduma ya haraka ya jeraha na chanjo inaweza kuleta tofauti kati ya maisha na kifo. "Kuosha kidonda vizuri kwa sabuni na maji baada ya kugusana na mnyama anayeshukiwa kuwa na kichaa ni muhimu na kunaweza kuokoa maisha." anasemaDaktari Traore.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Cape Verde, Mauritius na Ushelisheli wafanikiwa kuangamiza surua na  rubela
Rais wa Sudan Kusini Kiir amrejesha makamu wa rais katika mabadiliko ya baraza la mawaziri
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao kutoka Al Fasher ya Sudan tangu kutwaliwa na RSF
Rais wa Tanzania amteua binti na mkwe wake katika Baraza la Mawaziri
Rais Samia amteua waziri mpya wa fedha, awaacha mawaziri wa mambo ya nje na madini madarakani
Tovuti za taasisi za serikali ya Kenya zashambuliwa
Mgodi waporomoka DRC na kuua watu wasiopungua 32
Wahamiaji 4 wafariki baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba makumi ya watu kuzama pwani ya Libya
Kikundi cha matabibu kinaripoti visa ya ubakaji wa wasichana wa Al Fasher baada ya RSF kuteka
Mlipuko wa virusi vya Marburg umethibitishwa kusini mwa Ethiopia
DR Congo, M23 wasaini makubaliano ya amani 'ya kihistoria' nchini Qatar
Baraza la Maaskofu Tanzania lataka uwajibikaji kwa waliohusika na mauaji ya waandamanaji
Baraza la usalama la UN laongezea mwaka mmoja ujumbe wa amani wa Abyei
Kiongozi wa zamani wa waasi wa DRC anayeshtakiwa Paris kwa uhalifu wa kivita aanza mgomo wa kula
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano