| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Pep Guardiola ameishiwa makali yake Man City?
Mancjester City sasa wameshinda mechi 2 tu kati ya mechi 7 walizocheza, hali inayoongeza shinikizo kwa Pep Guardiola.
Pep Guardiola ameishiwa makali yake Man City?
Maswali yanaanza kuibuka iwapo Pep Guardiola ataendelea kuwa kocha wa timu ya Manchester City msimu ujao. / / Reuters
21 Januari 2026

Manchester City wamepata kichapo cha mbwa koko baada ya kuadhibiwa na timu ya kutoka Norway, Bodo/Glimt.

Timu hiyo imeizaba Man City 3–1 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

City sasa wameshinda mechi 2 tu kati ya walizocheza, hali inayoongeza shinikizo kwa Pep Guardiola.

“Tunahitaji kufanya vizuri,” alisema Pep Guardiola baada ya mechi. “Matokeo haya si mazuri.”

Cha kushangaza zaidi, Bodo/Glimt walikuwa hawajawahi hata kushinda mechi ya michuano hiyo ya Ulaya kabla ya mchezo huu.

Aidha mji wanaotoka timu hiyo una idadi ya watu tarkriban 55,000 tu, idadi inayotosha kujaza uwanja wa nyumbani wa Man City wa Etihad.

Maswali yanaanza kuibuka iwapo je, Pep bado ana makali, au huu ndio mwisho wa ubunifu wake Manchester City?

CHANZO:TRT Afrika