UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan kuhusu UNGA: Suala la Palestina lilitawala, Israel ilisahaulika, kikao na Trump kinatia moyo
Hakuna aliye tayari kusimama na Israel au kuonekana kwenye picha na serikali ya Netanyahu, isipokuwa mataifa machache,' anasema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Erdogan kuhusu UNGA: Suala la Palestina lilitawala, Israel ilisahaulika, kikao na Trump kinatia moyo
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan./Picha:AA
29 Septemba 2025

Rais wa Uturuki aliweka msisitizo kwenye umuhimu wa vuguvugu la Palestina wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, akisema, “pamoja na jitihada za kulizuia,  vuguvugu hilo limeacha alama katika mkutano huo wa 80."

“Hakuna aliye tayari kusimama na Israel au kuonekana kwenye picha na serikali ya Netanyahu, isipokuwa mataifa machache," alisema Recep Tayyip Erdogan katika hutoba yake kwa taifa baada ya kikao cha baraza la mawaziri.

Akipongeza orodha ya nchi zilizoitambua Palestina ambazo zimefikia 158, Erdogan alisema kuwa "tunafarajika sana kama taifa lenye kuongoza mapambano haya."

Kulingana na Erdogan, Uturuki inasimama na Wapalestina katika kulinda ardhi, uhuru na utu wao.

"Licha ya kucheleweshwa, utambuzi wa dola ya Palestina na wajumbe wawili wa baraza la usalama ni jambo muhimu sana,” aliongeza.

" Walau kila mtu anakubali kuwa Netanyahu anachochea vurugu za ulimwengu na kikanda akibakia madarakani huku kukiwa na uchunguzi wa ufisadi," alisema Erdogan.

Akizungumzia kikao chake cha wiki iliyopita alichofanya na Rais wa Marekani Trump, Rais Erdogan alisema: "Nina imani kuwa tutaona matokeo chanya ya mkutano huo katika siku zijazo.”

 

CHANZO:Anadolu Agency