tokea masaa 13
Watu wapatao 50 walipoteza maisha mwezi Januari, kufuatia mapigano kati ya wanamgambo wa serikali na vikundi vya waasi nchini DRC.
Kulingana na ripoti ya Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA), mauaji hayo yalitokea kati ya Januari 12 na 16 mwaka huu, katika eneo la Rutshuru, na kuathiri makundi ya Bukombo, Kihondo, Mutanda, Bambo na Tongo.
Watu kadhaa wanaripotiwa kujeruhiwa na wengine wengi kulazimika kuyahama makazi yao na kuelekea eneo la Masisi.
ZILIZOPENDEKEZWA
Katika tukio lingine, watu 11 waliuwawa na wengine 40 kujeruhiwa katika shambulizi la anga lililofanywa dhidi ya ngome za waasi mwanzoni mwa mwezi Januari, kulingana na ripoti ya OCHA.
CHANZO:AA





















