| Swahili
ULIMWENGU
3 DK KUSOMA
Bunge la Uganda yapitisha sheria ya kupambana na dawa za kulevya
Hii inakuja baada ya Shirikisho linalopambana na madawa ya kusisimua misuli duniani yaani World Anti-Doping Agency kubaini Sheria ya taifa ya Michezo Uganda halifanyi Shirika la Uganda la Kupambana na Madawa ya kuongeza nguvu kuwa huru.
Bunge la Uganda yapitisha sheria ya kupambana na dawa za kulevya
Bunge ya Uganda limepitisha Sheria ya Marekebisho ya Michezo ya Kitaifa / Picha: AP / Others
20 Desemba 2024

Bunge ya Uganda limepitisha Sheria ya Marekebisho ya Michezo ya Kitaifa, 2024 ili kuthibitisha uhuru wa Shirika la Uganda la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu.

Hii ni kwa nia ya kufanya chombo hicho kuwa huru.

Hili linakuja baada ya Shirikisho linalopambana na madawa ya kusisimua misuli duniani yaani World Anti-doping Agency, kubaini vifungu vilivyopitishwa katika Sheria ya Taifa ya Michezo havifanyi shirika la Uganda la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu kuwa huru.

"Baada ya kupeleka muswada huo katika Jumuiya ya Kimataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, walitaka baadhi ya mambo yawekwe bayana katika muswada huo," Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kiwanuka Kiryowa aliliambia Bunge.

"Walihitaji kuwa lazima kuwe na uwazi juu ya suala la uhuru wa Shirika la Uganda la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu. Walisema kwamba tunahitaji kusema wazi kwamba ni huru,” amesema Mwanasheria Mkuu, Kiryowa.

Shirikisho linalopambana na madawa kusisimua misuli duniani, lilikuwa linatishia kuwazuia wanariadha wa Uganda kushiriki katika michezo ya kimataifa iwapo Uganda itashindwa kuainisha sheria zake katika ngazi ya kimataifa.

"Tishio la kusimamishwa ni hitaji la dharura la kuainisha Sheria ya Kitaifa ya Michezo na Kanuni za Dunia za Kupambana na Dawa za Kulevya na Mkataba wa kimataifa wa UNESCO dhidi ya dawa za kuongeza nguvu."

Waziri wa nchi wa Michezo Ogwang Ogwang alitetea kupitishwa kwa muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Michezo ya Kitaifa, 2024 akisema uliundwa kushughulikia mapungufu katika Sheria ya Michezo ya Kitaifa, inayohusiana na kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

"Uganda inapaswa kutii hitaji hili kwa haraka, tunaweza kupoteza haki za uenyeji wa CHAN, AFCON na mashindano mengine ya kimataifa," Ogwanga aliliambia Bunge.

Alisema ingawa Uganda iliridhia Mkataba wa Kimataifa wa UNESCO dhidi ya matumizi ya dawa mbovu katika Michezo mnamo Mei 30, 2007, hata hivyo masharti katika Sheria ya Kitaifa ya Michezo yanayohusiana na kupinga matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini na hayaambatani na Kanuni ya Dunia ya Kupambana na Dawa za Kulevya.

CHANZO:TRT Afrika