Wanaovaa sketi fupi, suruali za kubana wapigwa faini Tanzania

Wanaovaa sketi fupi, suruali za kubana wapigwa faini Tanzania

Katika kijiji cha Arumeru Tanzania, wanaovaa sketi fupi, suruali za kubana au herini watapigwa faini ya TSh50,000. Pia kijana yeyote mwenye nguvu amepigwa marufuku kutofanya kazi na pia akionekana kuzurura asubuhi bila kazi atapigwa faini ya Sh50,000 nchini Tanzania. Vijana wa kiume pia wamepigwa marufuku kusuka nywele, kunyoa upande mmoja wa kichwa na kubakisha nywele katikati ya kichwa maarufu kiduku.