| swahili
AFRIKA
5 DK KUSOMA
DRC inapambana kuwa tayari kwa michezo ya Francophone
Ikiwa imesalia chini ya wiki moja kabla ya Michezo ya Julai 28 ya Francophone nchini DRC, nchi hiyo inapambana kujitayarisha kwa ajili ya mashindano hayo
DRC inapambana kuwa tayari kwa michezo ya Francophone
Uwanja wa Stade des Martyrs mjini Kinshasa, DRC utakuwa muhimu katika kuandaa Michezo ya Francophone Julai/ Picha: Reuters /
22 Julai 2023

Ikiwa imesalia wiki moja tu kabla ya sherehe za ufunguzi ya Michezo ya tisa ya Francophone.

Wafanyakazi huko Kinshasa wanajitahidi kumaliza maandalizi kabla ya michezo hiyo ambayo hukusanya mataifa kutoka jumuiya inayozungumza Kifaransa.

Takriban wanariadha 3,000 kutoka nchi 30 wanatarajiwa kuwasili Kinshasa, jiji kuu la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku chache zijazo kabla ya mchuano wa Julai 28.

Lakini wachoraji, mafundi na wafanyakazi wengine bado wanajitahidi kuandaa maeneo ya mashindano, na washiriki wengine wamejiondoa kwa sababu ya wasiwasi wa vifaa na usalama.

Mazoezi ya sherehe za ufunguzi hata hivyo yameanza katika uwanja wa Stade des Martyrs, ambao AFP iliutembelea wakati wa ziara iliyoandaliwa wanahabari na mabalozi wa kigeni siku ya Alhamisi.

"Ni dakika ya mwisho," alisema mgeni mmoja, ambaye alitabiri hata hivyo kwamba Michezo ingeendelea.

Hofu ya hafla kutofanyika

Hofu ya awali kwamba hafla hiyo ya siku 10 itasitishwa inaonekana kupungua.

DRC ilichaguliwa 2019 kama mwenyeji wa Michezo ya tisa ya Francophone, shindano lilanlofanyika kila baada ya miaka minne na inahusisha michezo na utamaduni.

Hapo awali michezo hiyo ilipangwa kufanyika mnamo 2021, lakini iliahirishwa kwa sababu ya janga la Covid na ikacheleweshwa tena mwaka jana kwa sababu vifaa havikuwa tayari.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Christophe Lutundula aliwaambia waandishi wa habari kwamba kupata fedha ya kuandaa hafla ya kimataifa ya michezo ni vigumu, "unapokuwa nchi iliyo kwenye vita."

Makundi yenye silaha yanakumba sehemu kubwa ya mashariki ya taifa hilo kubwa, na kusababisha vita ambavyo vilipamba moto katika miaka ya 1990 na 2000.

Kundi moja kama hilo, linalojulikana kama M23, limeteka maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini tangu lilipoibuka tena kutoka kwa makazi mwishoni mwa 2021, na kuwahamisha zaidi ya watu milioni moja.

Pesa

Kuandaa tu michezo hiyo kutagharimu makumi ya mamilioni ya dola. DRC pia imelazimika kujenga viwanja vya mpira wa vikapu, tenisi na judo, kuweka maeneo mapya ya soka na riadha na kuimarisha viwanja vilivyosahaulika kwa muda mrefu.

Katika uwanja mdogo karibu na Stade des Martyrs, uwanja ni mpya.

Kama wanariadha wengine wa Kongo, mwanariadha Francoise mwenye umri wa miaka 21 alifurahishwa na nchi yake kuleta vifaa vya kisasa.

"Mimi hukimbia kwenye udongo. Ni lazima nizoee," alisema.

Uwanja mwingine unaoitwa Tata Raphael wa Kinshasa uko katika hali mbaya.

Hali ni tofauti sana ikilinganishwa na siku yake ya kifahari ilikuwa 1974 wakati pambano maarufu la ndondi kati ya Muhammad Ali na George Foreman ulifanyika hapo.

Uwanja huo unatarajiwa kuwa "kijiji cha michezo", kulingana na mkurugenzi wa kamati ya maandalizi, Isidore Kwandja.

Kazi hapa imekuwa ya polepole kuliko katika Stade des Martyrs, lakini Kwandja alikuwa na imani kwamba kila kitu kitakuwa tayari kwa wakati.

Matatizo kuhusu fedha ya kuandaa michezo si ya DRC pekee.

Wiki hii, jimbo la Victoria la Australia lilijiondoa katika kuandaa Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2026, ikitaja gharama kubwa.

Afya na usalama

Wasiwasi kuhusu uhaba wa vituo vya afya, pamoja na usalama, tayari umesababisha baadhi ya wajumbe kusitisha ushiriki wao katika Michezo, au kutuma timu zenye idadi iliyopunguzwa sana.

Jimbo la Kanada la Quebec, kwa mfano, limejiondoa.

Mamlaka ya Kongo imesisitiza mara kwa mara kwamba vifaa vitakuwa tayari kwa wakati na kwamba michezo itakuwa salama.

Vikosi vya usalama tayari vimetumwa kwa vituo mbalimbali vya michezo kote jijini.

Kamati ya maandalizi ilisema ingawa kliniki ya afya iliyopangwa bado haijafunguliwa, vifaa vyote viko tayari, .

Na siku ya Alhamisi, kundi la waandishi wa habari na mabalozi walionyeshwa nusu dazeni ya ambulensi mpya ambazo zimetumwa.

Watangazaji tayari wanazunguka Kinshasa, wakipiga muziki kutoka kwa magari yao wakipigia debe michezo hii.

Lakini hali ni nzito kwa waandalizi wa michezo, kwasababu wiki iliyopita, mwanasiasa wa upinzani aliuawa katikati mwa Kinshasa.

Baadhi ya wanariadha waliofika jijini mapema wamelalamikia makazi yao kukosa maji.

CHANZO:TRT Afrika na mashirika ya habari
Soma zaidi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32
Ghana yafichua sababu ya ajali ya helikopta iliyoua watu wanane, wakiwemo mawaziri, mwezi Agosti
Nigeria yaanzisha uchunguzi baada ya kukamata kilo 1,000 za kokeini yenye thamani ya $235M
Kenya kuanzisha balozi zake mpya Vatican City, Denmark na Vietnam
Mtoto wa Gaddafi aachiliwa huru baada ya miaka kumi gerezani
Kuanzia vifo vya taratibu hadi mauaji ya ukatili: Kutoweka kwa utu Al Fasher
Zaidi ya mataifa 20 yanalaani ukatili wa RSF nchini Sudan, na kutaka kukomeshwa kwa ghasia
Rais wa Misri, afisa mkuu wa usalama wa Urusi kujadili ushirikiano wa kijeshi
Maelfu ya wananchi wanashikiliwa katika hali mbaya sana katika Al Fasher, Sudan: madaktari
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aghairi ziara iliyopangwa nchini Kenya
‘Mauaji ya waandamanaji ni chukizo mbele za Mungu’
Jeshi la Sudan lazima shambulio la RSF katika mji wa Babnousa huko Kordofan Magharibi
Majeshi ya Somalia yawaua viongozi watatu wakuu wa Al Shabaab
Rwanda, DRC zaanzisha mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi huku kukiwa na mazungumzo ya amani
RSF yazika miili katika makaburi ya halaiki, inachoma wengine ili 'kuficha ushahidi wa mauaji
Wananchi katika Al Fasher, Sudan, wanakabiliwa na ukatili 'wa kiwango kisichoweza kuaminika' — UN
Chama tawala nchini Djibouti kimemteua Rais Guelleh kwa muhula wa sita
Amaan Golugwa akamatwa huku polisi Tanzania ikiwasaka viongozi wa upinzani kufuatia maandamano
Wafanyakazi waokolewa baada ya maharamia kushambulia meli ya mafuta kutoka Somalia