Rais wa Uturuki aRecep Tayyip Erdogan alifanya mazungumzo ya simu na rais wa Marekani Donald Trump siku ya Ijumaa, kufuatia ombi la Washington, kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.
Viongozi hao, walijadiliana uhusiano wa nchi zao na hali halisi ya Gaza.
Erdogan aligusia kuwa, ziara yake ya hivi karibuni nchini Marekani, iliimarisha uhusiano, akisisitizia umuhimu wa kukuza ushirikiano katika nyanja mbalimbali, hususani ulinzi.
Kuhusu suala la Gaza, Erdogan alisema kuwa Uturuki inafanya jitihada ya kukuza amani na utulivu sio katika eneo la Gaza lakini katika ukanda mzima.
Alipongeza jitihada mbalimbali za kimataifa za kufikia lengo hilo, akisema kuwa Uturuki imeongeza kasi yake ya kidiplomasia ili amani ipatikane.
Kulingana na rais huyo wa Uturuki, ni muhimu Israel iache mashambulizi yake ili kufanikisha lengo la kupatikana kwa amani ya kikanda.