2 Oktoba 2025
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, siku ya Alhamisi alifanya kumbukumbu ya miaka 838 ya kutwaliwa kwa mji wa Yerusalem.
"Katika kumbukumbu hii ya miaka 838, kwa kipekee namkumbuka Saladin Ayyubi na askari zake mashujaa," alisema Erdogan kupitia mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal.
Wakati huo huo, Erdogan alionesha nia thabiti ya kuipambania Yerusalem, akisema kuwa ni urithi kutoka kwa Mtume Muhammad na manabii waliomfuatia.
Yerusalem, pia ikijulikana kama Quds, ni mji wa kwanza wa qibla kwa Waislamu na huchukuliwa kama mji wa tatu Mtakatifu, baada ya Mecca na Medina.
CHANZO:AA