UTURUKI
1 dk kusoma
Rais Erdogan wa Uturuki alaani shambulizi la Israel dhidi ya msafara wa kupeleka misaada Gaza
"Netanyahu, ambaye ni muuaji wa kimbari anashindwa hata kutoa nafasi kwa ajili ya amani," anasema Rais wa Uturuki Erdogan.
Rais Erdogan wa Uturuki alaani shambulizi la Israel dhidi ya msafara wa kupeleka misaada Gaza
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan./Picha:AA
2 Oktoba 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani “vitendo vya kiharamia” dhidi ya misafara ya kibinadamu inayoelekea Gaza kuwasaidia Wapalestina “wanaonyanyaswa”.

Katika hotuba yake ya Alhamisi wakati wa kikao cha wakuu wa chama cha AK, Erdogan alisema kuwa shambulizi hilo ni ishara kuwa mifumo ya mauaji ya kimbari inaendelea kuficha uhalifu wake huko Gaza.

"Netanyahu, ambaye ni muuaji wa kimbari anashindwa hata kutoa nafasi kwa ajili ya amani," anasema Rais wa Uturuki Erdogan.

Kulingana na rais huyo wa Uturuki, msafara wa Sumud umedhihirisha “uovu unaoendelea Gaza na sura ya kiuaji ya Israel.”

"Hatutowaacha ndugu zetu wa Palestina na tutatumia uwezo wetu kuhakikisha kuwa amani inapatikana," alisema.

Kulingana na Erdogan, mamlaka za Uturuki zinaendelea kufuatilia kinachoendelea na kuchukua hatua stahiki kukakikisha kuwa raia walio kwenye misafara hiyo hawadhuriki.

CHANZO:AA