| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mshambuliaji wa Algeria awaomba radhi mashabiki wa DRC
Mshambuliaji wa Algeria, Mohamed Amoura, ameomba radhi kufuatia ishara tata aliyoifanya wakati wa kusherehekea ushindi wa timu yake dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.
Mshambuliaji wa Algeria awaomba radhi mashabiki wa DRC
Amoura amesema hakujua umuhimu wa yule mtu aliyekuwa jukwaani. Naomba radhi kwa mashabiki wa Congo. / / User Upload
8 Januari 2026

Ishara hiyo ilitafsiriwa na mashabiki wengi kuwa ya kudhalilisha. Amoura amesema hakujua maana halisi ya ishara hiyo na anasikitishwa na sintofahamu iliyojitokeza.Mashabiki wengi waliitafsiri ishara hiyo kama kejeli dhidi ya Michel Nkuka Mboladinga, shabiki wa DRC almaarufu “Lumumba Vea.”

“Nilikua na hisia kali sana wakati huo na sikujua umuhimu wa yule mtu aliyekuwa jukwaani. Naomba radhi kwa mashabiki wa Congo,” Amoura aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

“Ninaiheshimu Congo na timu yao. Kwa dhati kabisa nawatakia kila la heri na natumaini watafanikiwa kufuzu Kombe la Dunia. Ikiwa tabia yangu ilieleweka vibaya, naomba radhi kwa moyo wote kwa sababu haikuwa dhamira yangu hata kidogo,” alisema.

CHANZO:TRT Afrika