AFRIKA
1 dk kusoma
Kiongozi wa Mali awafuta kazi makamanda waandamizi huku kukiwa na matatizo ya usalama
Kiongozi wa mpito wa nchi hiyo Assimi Goita alimtimua naibu kamanda wa jeshi, mkuu wa usalama jeshini na mkuu wa majeshi ya ardhini.
Kiongozi wa Mali awafuta kazi makamanda waandamizi huku kukiwa na matatizo ya usalama
Assimi Goita aliingia madarakani Juni 7, 2021. / Wengine
tokea masaa 7

Rais wa mpito wa Mali amewafuta kazi makamanda watatu waandamizi wa jeshi, taarifa kutoka kwa baraza la mawaziri zimeonesha siku ya Jumatano.

Rais Assimi Goita amemtimua naibu kamanda wa jeshi, mkuu wa usalama jeshini na mkuu wa majeshi ardhini, taarifa hiyo ilisema.

Shirika la AFP limearifu kuwa watatu hao walifutwa kwa "utendakazi mbaya" katika uwanja wa vita, wakimtaja afisa mmoja mwandamizi.

Tangu 2012 Mali imekuwa na matatizo ya kiusalama kutokana na mashambulizi ya magaidi wenye uhusiano na makundi ya Al Qaeda na Daesh.

Goita aliingia madarakani kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya 2020 na 2021 akiahidi kuimarisha usalama.

Katika siku za hivi karibuni magaidi wanaohusishwa na Al Qaeda wamekuwa wakitaka kuleta hatari mji mkuu, Bamako kwa kuzidisha mashambulizi katika maeneo ya karibu.

Tangu Septemba wamekuwa wakizuia mafuta kuingia nchini kutoka mataifa jirani, jambo linalosababisha matatizo kwa watu kwenye taifa hailo ambalo halina bandari.

CHANZO:TRT Afrika Swahili