tokea masaa 11
Dar es Salaam, ambalo ni jiji la kibiashara limetatizika zaidi baada ya polisi kutangaza amri ya kutotoka majumbani kuanzia saa kumi na mbili jioni. Hii ni baada ya waandamanaji kujitokeza barabarani na baadhi yao kuharibu majengo ikiwemo kuchoma moto kituo cha polisi.
Kutokana na hali hii maeneo mengi ya biashara yamefungwa huku polisi na jeshi wakionekana wakishika doria au kuwepo katika baadhi ya sehemu.
Nchi pia imekumbwa na kusitishwa kwa intaneti kote, jambo lililotatiza utoaji huduma ikiwemo kutumia usafiri wa umma. Watumishi wa umma wameagizwa kufanyia kazi kutoka majumbani.
CHANZO:TRT Afrika Swahili









