AFRIKA
2 dk kusoma
Kiongozi wa Al-Shabab miongoni mwa magaidi 24 waliouawa Somalia
Maafisa wa usalama wa Somalia wanasema wameratibu operesheni iliyowalenga viongozi wa al-Shabab na magaidi wengine, na kuwaua magaidi 24.
Kiongozi wa Al-Shabab miongoni mwa magaidi 24 waliouawa Somalia
Kundi la al-Shabab limekuwa likitekeleza ugaidi dhidi ya serikali ya Somalia kwa miaka kadhaa. / Picha: Reuters
tokea masaa 3

Shirika la Kijasusi la Somalia (NISA) siku ya Alhamisi lilifanya mashambulizi yaliyowalenga viongozi wa al-Shabab na magaidi wengine, na kuwaua magaidi 24.

Operesheni hiyo ilifanyika kwa ushirikiano wa washirika wa usalama wa kimataifa katika mikoa ya Hiran, Galgadud, na Lower Shabelle.

Abdi Hiray, ambaye amekuwa akifuatiliwa na idara ya ujasusi kwa muda mrefu, alikuwa miongoni mwa wale waliouawa katika operesheni hiyo eneo la Hiran, huku magaidi wengine 21 wakiuawa katika kijiji cha Tugarey eneo la Lower Shabelle na lile la kati la Galgadud, kulingana na taarifa kutoka kwa shirika hilo la ujasusi NISA.

Hiray alihusika na njama na mashambulizi kadhaa yaliyosababisha madhara kwa raia katika jimbo la kusini kati la Hirshabelle, NISA ilisema.

Serikali yazidisha mapambano dhidi ya al-Shabab

“Operesheni hizi ni sehemu za juhudi zinazoendelea kulemaza kundi la Khawarij na kuzuia njama zozote mbaya dhidi ya watu wa Somalia,” taarifa hiyo ilisema.

Khawarij ni neno ambalo serikali ya Somalia hutumia kuzungumzia kundi la kigaidi la al-shabab lenye ushirikiano na al-Qaeda.

Tangu mwezi Julai, jeshi la Somalia, kwa msaada wa AUSSOM na washirika wengine wa kimataifa, limezidisha operesheni dhidi ya kundi hilo la kigaidi lenye ushirikiano na al-Qaeda katika mikoa ya kusini na kati ya Somalia.

Al-Shabab, ambayo imekuwa ikitekeleza ugaidi dhidi ya serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16, mara nyingi inalenga vikosi vya usalama, maafisa, na raia.

CHANZO:AA