| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Katibu Mkuu wa kwanza wa EAC Edwin Mtei kuzikwa Januari 24
Kulingana na Mashinda Mtei, ambaye ni mtoto wa Gavana huyo wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mzee Mtei anatarajiwa kupumzishwa katika kata ya Ambureni, eneo la Tengeru, Arusha, Jumamosi ya Januari 24.
Katibu Mkuu wa kwanza wa EAC Edwin Mtei kuzikwa Januari 24
Aliyekuwa Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Mzee Edwin Mtei./Picha:@jumuiya
20 Januari 2026

Katibu Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki, Edwin Mtei anatarajiwa kuzikwa jijini Arusha nchini Tanzania, Jumamosi ya Januari 24, 2026.

Kulingana na Mashinda Mtei, ambaye ni mtoto wa tatu wa Mzee Mtei,  Gavana huyo wa kwanza wa Benki kuu ya Tanzania (BOT), na Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), atazikwa katika kata ya Ambureni Eneo la Tengeru Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Akizungumzia kifo cha baba yake mapema Januari 20, Mashinda alisema Mzee Mtei amefariki kwa uzee, akiongeza kuwa, alishindwa hata kuzungumza kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kutokana na umri wake.

Mapema Januari 20, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Veronica Nduva, aliongoza wafanyakazi wa sekratariati ya Jumuiya hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha, kumkumbuka Mzee Mtei, ambaye ndiye Katibu Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuvunjika mwaka 1977.

Mzee Mtei alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, kuanzia mwaka 1967 hadi 1971.

Katika kumbukumbu hiyo fupi, Nduva alimuelezea Mzee Mtei kama kiongozi hodari aliyeweka misingi ya ushirikiano wa kikanda na utangamano wa Afrika Mashariki, akiacha nyuma urithi ambao utaendelea kuongeza ushawishi mkubwa kwa vizazi vya Afrika Mashariki na kwingineko.

Mzee Mtei amefariki dunia usiku wa kuamkia Januari 20, akiwa na umri wa miaka 94.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Rais wa Congo-Brazzaville mwenye umri wa miaka 82 anasema hatokuwa madarakani 'milele'
Shambulio la droni la RSF lasababisha kukatika kwa umeme katika eneo la  El-Obeid ya Sudan
Somalia yazindua kitambulisho cha kitaifa kwa usafiri wa ndani
Mvutano wa Mashariki ya Kati unalazimisha safari za meli duniani kote kuzunguka Afrika
Nchi za Kiafrika zinaendelea kuwalinda raia wao katikati ya mzozo wa Mashariki ya Kati
Jeshi la Somalia, vikosi vya Uganda vyashambulia magaidia wa Al Shabab
Mbunge wa Kenya miongoni mwa watu sita waliouawa katika ajali ya helikopta
Nigeria, Senegal, Libya wanaomba kujizuia katikati ya mashambulizi ya Marekani-Israel dhidi ya Iran
Raia wafurika mitaa ya Iran baada ya mashambulizi ya Israel na Marekani kumuua Ali Khamenei
Waziri wa zamani wa fedha wa Sudan Kusini alikamatwa akijaribu kukimbia nchi
Kampeni za uchaguzi wa urais zaanza nchini Jamhuri ya Congo
Umoja wa Afrika watoa wito wa 'kupunguzwa uhasama' baada ya Marekani na Israel kushambulia Iran
Mchengerwa: Tanzania haina mgonjwa wa Uviko-19
Shambulio la Iran linakuja wakati wa mazungumzo ya nyuklia. Nini kitatokea baadaye?
Israel yaanza mashambulizi dhidi ya Iran licha ya mazungumzo na Marekani
Zaidi ya raia 50 wa Ghana wameuawa katika vita nchini Ukraine
Sudan Kusini inahitaji “hatua za dharura” ili kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
Rais wa Burkina Faso asaini mkataba wa afya wenye utata unaofadhiliwa na serikali ya Trump
Wakimbizi wa Burundi warudi kutoka Tanzania
Ramadhan mjini Mombasa: Utamaduni, fursa na mabadiliko ya kijamii