AFRIKA
1 dk kusoma
Ethiopia imeonesha nia ya kuandaa mashindano ya Riadha ya Dunia
Shirikisho la Riadha la Ethiopia linasisitiza kuwa Ethiopia ina vifaa bora vya michezo, vituo vya mafunzo, hoteli, usafiri wa anga na ardhini, na miundombinu mingine muhimu ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika
Ethiopia imeonesha nia ya kuandaa mashindano ya Riadha ya Dunia
Ethiopia inatambuliwa duniani kwa kuwa na wanariadha bora / picha: AP
19 Septemba 2025

Ethiopia imewasilisha rasmi ombi kwa Shirika la Wanariadha wa Dunia kutaka kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha ya Dunia mwaka wa 2029 au 2031.

Wawakilishi wa serikali na maofisa kutoka Shirikisho la Riadha la Ethiopia (EAF) walihudhuria Mpango wa Waangalizi huko Tokyo, ambapo walifanya mijadala na kubadilishana uzoefu na wajumbe kutoka nchi nyingine walio na nia ya kuandaa mashindano hayo.

Meku Mohammed, Waziri wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Utamaduni na Michezo, alisema kuwa kwa kipeke serikali inatoa kipaombele na rasilimali kwa sekta ya riadha.

Alibainisha kuwa Ethiopia imefanya kazi ya kujenga uwezo wake kwa kutatua changamoto zilizopo katika vifaa vya michezo na kujenga viwanja vipya.

"Serikali imejitolea kurejesha riadha katika hadhi na uhai wake wa awali," Meku alisema.

Sileshi Sihine, Rais wa EAF, alisisitiza utayari wa Ethiopia, akiangazia makali ya ushindani ya nchi katika suala la vifaa.

"Ethiopia ina vifaa bora vya michezo, vituo vya mafunzo, hoteli, usafiri wa anga na ardhini, na miundombinu mingine muhimu ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika," alisema.

Sileshi pia alisisitiza umuhimu wa kupata mafunzo kutoka kwa nchi zilizowahi kuandaa michuano hiyo.

CHANZO:TRT Swahili