| Swahili
Maoni
AFRIKA
3 dk kusoma
Kuteleza kwa Israel katika suala la Somaliland: Hatua itakayohatarisha usalama katika kanda
Ushirikiano wa Israel na Somaliland siyo tu kuteleza kimkakati lakini pia ni hatua mbaya kisiasa, ambayo badala ya kuimarisha uwezekano wake wa kutambulika kimataifa, inaiweka katika hatari ya kutengwa.
Kuteleza kwa Israel katika suala la Somaliland: Hatua itakayohatarisha usalama katika kanda
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akihutubia bunge la Somalia baada ya Israel kuitambua Somaliland kama taifa huru.
30 Desemba 2025

Abdiwahab Sheikh Abdisamad

Hatua ya Israel kuitambua Somaliland siyo ya kimkakati. Ni hatari zaidi ambayo inaweza kusababisha mgogoro katika enep na Pembe ya Afrika.

Badala ya kuleta usalama na mafanikio ya kidiplomasia. Hatua kama hizo zinaleta mgawanyiko zaidi, kuchochea vita, na kutatiza hali tete ya usalama.

Magawanyiko wa ndani

Kwa Israel kutambua Somaliland kunaweza kusababisha hali mbaya kwa watu, kuchochea taharuki iliopo kwa sasa na pengine kuwepo kwa migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.

Hali hiyo tete ina uwezekano wa kuwaondoa watu wengi katika makazi yao, kufanya kuwepo kwa changamoto za makazi, chakula, na misaada ya afya.

Jamii ya Kimataifa lazima ifuatilie kwa makini hali ilivyo ili kuepuka matatizo makubwa na kutoa misaada kwa jamii ambazo zinaathirika na vurugu."

Kuanzishwa kwa jimbo jipya la Kaskazini mashariki ndani ya Somaliland kumetatiza uwezekano wa kuwa na taifa lenye umoja la Somaliland kutambuliwa kimataifa kama taifa huru.

Katika eneo la Awdal, viongozi wa sehemu hiyo wanataka kuundwa kwa jimbo lao wenyewe ndani ya Jamhuri ya Somalia.

Kwa halii hii inamaanisha wakati Somaliland inatarajia kutambuliwa kimataifa, ndani ya nchi yenyewe kutakuwa na mgawanyiko mkubwa.

Zaidi ya hapo, ndani ya Somaliland kwenyewe kuna matatizo ya kikoo ambayo yanaweza kutatiza upatikanaji wa uhuru. Miongoni mwa koo kubwa tano, nne zinapendelea kuwa sehemu ya Somalia.

Hata ndani ya ukoo wa Isaaq, ambao ni sehemu kubwa ya watu wa Somaliland, wengi wao wanaunga mkono sera ya kuwa taifa moja. Ni idadi ndogo ya tabaka la wanasiasa,pamoja na mataifa ya nje wanaowaunga mkono, ndiyo wanataka kujitenga.

Kutambuliwa pia kunahatarisha suala la Palestina kukiwa na madai kuwa Israel itawapeleka Wapalestina milioni 1.5 na kuwaacha Somaliland, ili wasiangazie tena mzozo wa Israel na Palestina.

hatua kama hiyo inaweza kufanya iwe vigumu kwa Palestina kimataifa na kuzua wasiwasi wa kimaadili kuhusu watu kuondolewa kwenye makazi yao kwa lazima na kutilia shaka suala la usalama.

Hatua ya Israel huenda ikafanya kuwepo na muungano wa kitaifa, makubaliano hayo yanaweza kufanya waungane zaidi kisiasa na mipaka yao.

Kwa kumalizia, Israel kushirikiana na haikuwa tu kuteleza kimkakati bali hakuna msingi kisiasa, na sasa badala ya Somaliland kuimarisha kutambuliwa kimataifa, kunahatarisha ,kutengana na washirika muhimu katika kanda.

Pamoja na kuimarisha umoja wa Somalia bila kuwa na nia hiyo, kile ambacho kimedhamiriwa huenda ikawa imeleta mtafauruku zaidi katika Pembe ya Afrika,kudhihirisha mikakati isiyo ya msingi inaweza kutatizika na kuchochea ukosefu wa usalama.

Mwandishi, Abdiwahab Sheikh Abdisamad ni mchambuzi wa kisiasa ambaye utafiti unaangazia Pembe ya Afrika

Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

CHANZO:TRT Afrika