Takwimu zinaonyesha maambukizi takriban 300,000 ya kipindupindu na zaidi ya vifo 7,000, ongezeko la zaidi ya asilimia 30 kutoka mwaka uliopita.
Nchi za Angola na Burundi zimerekodi ongezeko kubwa la maambukizi kutokana na upatikanaji mdogo wa maji safi.
Hata hivyo, kituo hicho kimesema mlipuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaonekana kudhibitiwa, ingawa maeneo yenye migogoro bado yako hatarini, huku ugonjwa huo ukienea kwa haraka katika kambi zilizojaa watu na usafi duni.
Hata hivyo hali imeimarika katika nchi za Sudan Kusini na Somalia.
CDC ya Afrika ilisema kuwa Ethiopia imegundua watu wanane wanaoshukiwa kuwa na homa ya kuambukiza na inasubiri matokeo ili kubaini sababu haswa ya ugonjwa huo.
Aidha CDC ya Afrika ilisema mlipuko wa Mpox unapungua katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi lakini bado ni wasiwasi katika maeneo kama Kenya, Guinea, Liberia na Ghana.





















