Ofisi ya Mwenyekiti wa Shirika linlaohudumia Waturuki wanaoishi Ughaibuni na Jamii Husika (YTB) imezindua Kitabu cha Mwaka cha Afrika 2024, toleo jipya kabisa la uchapishaji wake wa kila mwaka linaoangazia maendeleo katika bara la Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya YTB, kitabu hicho ni tathmini ya kila mwaka ya Uturuki kuhusu Afrika, ikitoa muhtasari wa kina na wa kimfumo kuhusu maendeleo ya kisiasa, kiuchumi, kijeshi, kiteknolojia, kimazingira na kijamii barani humo.
Kitabu hicho, ambacho kilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2022 na kinapatikana kwa lugha ya Kituruki na Kiingereza, pia kinamulika ajenda chanya katika bara la Afrika, zikiwemo hatua zilizopigwa katika elimu, utamaduni, sanaa, michezo, sinema na muziki.
Toleo la mwaka huu lina vipengele vitano vikuu: Siasa, Uchumi, Jamii na Mazingira; Mahusiano ya Uturuki na Afrika; Mahusiano ya Wadau wa Kikanda, Kimataifa na Afrika; Utamaduni, Sanaa, Elimu na Michezo; pamoja na machapisho kuhusu Afrika.
Athari za kimataifa
Kitabu hiki pia kinajadili matukio yenye athari kubwa duniani, ikiwemo utatuzi wa mgogoro kati ya Somalia na Ethiopia kupitia usuluhishi wa Uturuki mwaka 2024, pamoja na kesi ya mauaji ya halaiki iliyofunguliwa dhidi ya Israel na nchi ya Afrika Kusini.
Kwa jumla, kitabu hichi kina makala 12 za kitaasisi na michango kutoka kwa waandishi 53, ikiweka pamoja jumla ya makala 66 na tathmini ya vitabu 9. Toleo hili linaanza na dibaji iliyoandikwa na Emine Erdoğan, mke wa rais wa Uturuki.
YTB inaeleza kuwa kitabu hiki kina lengo la kuwezesha tathmini ya kina na ya kimkakati kuhusu mahusiano kati ya Uturuki na Afrika.
Miongoni mwa wachangiaji ni taasisi kuu za kitaifa kama Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Ulinzi, Ofisi ya Masuala ya Kidini, Taasisi ya Yunus Emre (YEE), Shirika la Ushirikiano na Uratibu la Uturuki (TİKA), Taasisi ya Maarif, Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuku, Shirika la Habari la Anadolu, Shirika la Utangazaji la TRT, Baraza la Mahusiano ya Kiuchumi ya Nje (DEİK), na Shirika la Ndege la Uturuki.
Mbali na uchambuzi wa kisekta, chapisho hili linaangazia pia matukio ya kimataifa yenye athari kubwa kwa Afrika, yakiwemo usuluhishi uliofanywa na Uturuki uliosaidia kupunguza mvutano kati ya Somalia na Ethiopia mwaka 2024, pamoja na kesi ya mauaji ya halaiki iliyofunguliwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel.



























