Makamu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Wegesa Heche anatarajiwa kuongoza viongozi wengine wa chama hicho kwenye mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho iliyotolewa Oktoba 17, 2025, Heche ataambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema pamoja na Boniface Jacob (Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani), kwenda kijijini Bondo, ambapo mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe yatafanyika Oktoba 19, 2025.
Msafara huo utakwenda baada ya mazungumzo yaliyofanywa na Mwenyekiti CHADEMA taifa, Tundu Antiphas Lissu na Heche mahakamani, siku ya Oktoba 16, 2025.
Katika mazungumzo hayo, Lissu ambaye yuko rumande akikabiliwa na tuhuma za Uhaini, alikielekeza chama chake kwenda Kenya, kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe.
Odinga alifariki dunia ghafla Oktoba 15, 2025 nchini India, alipokuwa akipatiwa matibabu.