Watanzania kumjua Rais wao mpya ndani ya saa 72
Raia wa Tanzania kutoka sehemu mbalimbali za nchi wameanza kupiga kura mapema hii. Zoezi hilo limeanza rasmi saa moja asubuhi na linatarajiwa kukamilika saa kumi alasiri.
Watanzania kumjua Rais wao mpya ndani ya saa 72
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, INEC, Ramadhan Kailima / Public domain
tokea masaa 13

Huku mchakato wa upigaji kura ukiendelea katika maeneo tofauti nchini Tanzania, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (INEC), imeweka wazi kuwa itamtangaza mshindi wa kiti cha urais ndani ya siku tatu.

Kulingana na Mkurugenzi wa INEC, Ramadhan Kailima, tume hiyo itamtangaza Rais mpya ndani ya saa 72, ikiahidi uwazi, haki na uadilifu katika mchakato huo.

Kailima alisisitiza kuwa tume hiyo inatangaza matokeo hayo kwa wakati.

“INEC imekamilisha maandalizi yote muhimu ya uchaguzi, na tunawahakikishia Watanzania kuwa matokeo ya urais yatatangazwa ndani ya saa 72 baada ya zoezi la upigaji kura,” alisema Kailima.

Kwa mujibu wa Kailima, ofisi yake imejipanga kuhakikisha uwazi na ufanisi katika kusimamia uchaguzi huru na wa haki.

“Tume itaratibu ukusanyaji na uhakiki wa matokeo kwa ngazi zote kwa wakati, kuanzia vituo vya majimbo hadi makao makuu, na ndani ya saa 48 hadi 72 matokeo yatakuwa yametangazwa.

Matokeo ya madiwani na wabunge yatatangazwa muda wowote baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika vituoni, tume itapokea matokeo ya urais na kufanya majumuisho kwa muda ulioapangwa,” aliongeza Kailima.

Raia wa Tanzania kutoka sehemu mbalimbali za nchi wameanza kupiga kura mapema hii. Zoezi hilo limeanza rasmi saa moja asubuhi na linatarajiwa kukamilika saa kumi alasiri.

CHANZO:TRT Swahili