| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Senegal yakata rufaa katika mahakama ya CAS kupinga kunyang’anywa ubingwa wa AFCON
Senegal imekata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kupinga uamuzi wa kunyang’anywa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika na kukabidhiwa kombe hilo Morocco.
Senegal yakata rufaa katika mahakama ya CAS kupinga kunyang’anywa ubingwa wa AFCON
Senegal wanataka kurudisha taji lao la pili la AFCON baada ya CAF kubatilisha ushindi wao wa AFCON 2025. / / AP
tokea masaa 4

Mahakama hiyo yenye makao yake Uswizi ilithibitisha siku ya Jumatano kwamba Senegal imewasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo.

“Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) inathibitisha kupokea rufaa kutoka Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) dhidi ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Morocco,” CAS iliandika katika taarifa.

Senegal wanataraji kubatilisha uamuzi wa shirikisho la soka barani Afrika wa kuwanyang’anya taji hilo baada ya baadhi ya wachezaji wao kutoka nje ya uwanja wakipinga penalti iliyotolewa kwa Morocco wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika tarehe 18 Januari, mchezo ambao Senegal walishinda 1-0 katika muda wa nyongeza.

CAF ilitangaza tarehe 17 Machi kuwa imekubali rufaa ya Shirikisho la Soka la Morocco, ikisema kuwa Senegal walikiuka kanuni za mashindano kwa kutoka nje ya uwanja.

CAS yaahidi uamuzi wa haraka

Kwa yaliyojiri, CAF ilitangaza kuwa Senegal walipoteza mechi hiyo kwa kujiondoa uwanjani, hivyo ushindi wao wa 1-0 ukageuzwa kuwa kipigo cha 3-0, na kuwafanya wenyeji Morocco kuwa mabingwa.

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ilisema rufaa ya Senegal “inalenga kufuta uamuzi wa CAF na kuitangaza FSF kuwa washindi wa AFCON.”

Mkurugenzi Mkuu wa CAS, Matthieu Reeb, aliongeza: “Tunaelewa kuwa timu na mashabiki wanataka kujua uamuzi wa mwisho, na tutahakikisha mchakato wa usuluhishi unafanyika kwa haraka iwezekanavyo, huku tukiheshimu haki ya pande zote kusikilizwa kwa haki.”

CHANZO:AFP