| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mafuriko Kenya: Takriban watu 81 wafariki kutokana na mvua kali za wiki kadhaa
Sehemu kubwa ya Kenya imekumbwa na mvua kali kwa wiki kadhaa, huku mji mkuu wa Nairobi ukiathirika zaidi.
Mafuriko Kenya: Takriban watu 81 wafariki kutokana na mvua kali za wiki kadhaa
Mamlaka ya Hali ya Hewa imetahadharisha kuendelea kwa mvua. / AP
23 Machi 2026

Mvua na upepo mkali iliyoleta mafuriko nchini Kenya imesababisha vifo vya watu takriban 81 mwezi huu, mamlaka za nchi hiyo zimesema Jumapili, huku mvua zikiendelea kupiga sehemu kubwa ya nchi.

Katika maeneo ambayo yameathirika zaidi, wakazi walipita katika mafuriko wakibeba vitu vyao kichwani na kuokolewa kwa maboti.

Mafuriko yalifukia sehemu kubwa ya vijiji vya kaunti ya Kisumu, na kuharibu hekari 1,200 za mashamba na kuharibu mimea.

Zaidi ya familia 3,000 zimelazimika kuacha makazi yao katika eneo la Nyakach, huku baadhi waliotafuta hifadhi, wakisema kuwa ongezeko la maji kutoka Mto Mirui linaendelea kuhatarisha maisha.

"Tumepoteza sehemu kubwa ya mashamba kutokana na mmomonyoko, na mimea tuliyopanda," amesema chifu wa Nyakach, Oluoch Agwanda, 57.

Uharibifu mkubwa

Mji mkuu wa Nairobi una idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na mafuriko, ambapo watu 37 wamefariki, kwa mujibu wa mamlaka.

"Idadi inayoongezeka ya vifo kwa bahati mbaya imefikia 81," msemaji wa taifa wa polisi Muchiri Nyaga amesema katika taarifa.

"Kwa kuongezea, mafuriko yamesomba maeneo kadhaa, na kuacha takriban familia 2,690 bila makazi na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na mali.”

Mamlaka ya Hali ya Hewa inatabiri kuendelea kunyesha kwa mvua mpaka Jumanne, hivyo kutaka watu kuchukua tahadhari ya kutosha.

Watu wawili wanaripotiwa kuzama katika mafuriko mjini Kiambu, nje kidogo na mji mkuu, polisi imeiambia AFP.

Wawili pia walifariki katika maporomoko ya ardhi yaliyokumba kijiji cha magharibi cha Kasaka, kufukia nyumba kadhaa, imeripoti Citizen TV.