AFRIKA
1 dk kusoma
Samia: Vijana lindeni nchi yenu
Mgombea huyo wa CCM, alisisitiza kuwa amani ikivurugika vijana watashindwa kushiriki shughuli mbalimbali kama vile uchimbaji madini na burudani.
Samia: Vijana lindeni nchi yenu
Mgombea wa Urais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi./Picha:@ccm_tanzania
tokea masaa 9

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewataka vijana nchini humo, kuonesha uzalendo kwa nchi yao, waipende, walinde amani yake na kutokukubali kushawishiwa kuharibu amani hiyo.

“Vijana nawaomba tuwe wazalendo, tuipende nchi yetu. Hatuna nchi nyingine isipokuwa Tanzania, msije kuruhusu mtu akaja akasema fanyeni hili, fanyeni hivi. Sisi tunaipenda nchi yetu, nanyi muipende nchi yenu na muwe wazalendo,” alieleza Samia, ambaye pia ni Rais wa Tanzania, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Bukombe mkoani Geita.

Kulingana na Samia, kuna nchi mmoja tu duniani, iitwayo Tanzania, na toka kuundwa kwake, imepigana vita dhidi ya Idi Amin peke yake.

Samia aliongeza kuwa, nchi hiyo imebakiwa kuwa salama kwa miaka mingi, huku watu wan chi hiyo wakiendelea kuilinda tunu hiyo.

Mgombea huyo wa CCM, alisisitiza kuwa amani ikivurugika vijana hawatokwenda kuchimba madini na watashindwa kushiriki shughuli za burudani, iwapo amani itaharibika.

“Hivyo, amani hiyo mkiihatibu, ninyi mtwakwenda wapi wakati wao wanakuja kwetu? Kwa hiyo hakuna pakukimbilia isipokuwa hapa hapa kwetu,” alisema Rais huyo wa Tanzania.

CHANZO:TRT Afrika Swahili