AFRIKA
1 dk kusoma
ACT Wazalendo Zanzibar yaahidi kuwasaidia wavuvi
Othman alisikiliza kero za wananchi ikiwa ni pamoja na hofu ya kuhamishwa katika eneo hilo ili kupisha ujenzi wa soko.
ACT Wazalendo Zanzibar yaahidi kuwasaidia wavuvi
Othman Masoud Othman, mgombea urais Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo. / AA
tokea masaa 12

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya ACT wazalendo Othman Masoud Othman, ameahidi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Zanzibar kutowaondoa wajasiriamali wanaoanika dagaa huko Fungurefu Mkokotoni, na badala yake serikali itawawezesha kuzalisha kisasa.

Othman ameyasema hayo huko Fungurefu Mkokotoni Kaskazini A Unguja alipozungunza na wavuvi.

Katika ziara hiyo ya kampeni katika Jimbo la Tumbatu Kaskazini Unguja Othman alisikiliza kero za wananchi ikiwa ni pamoja na hofu ya kuhamishwa katika eneo hilo ili kupisha ujenzi wa soko.

Kwa upande wake, mgombea urais huyo wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, amesema kuwa sera ya chama chake ni kuhakikisha kwamba Wazanzibar wanasaidiwa, vifaa, elimu na kuwezeshwa kuzalisha kwa tija kwenye sekta mbali mbali ikiwemo ya uvuvi ili kuweza kuuza samaki na mazao mengine ya bahari ndani na nje ya nchi.