Kongamano hilo linawaleta pamoja viongozi wa nchi, waasisi wa biashara, wavumbuzi wa teknolojia, na mabalozi wa utamaduni —wakiangazia mikakati ya kuimarisha maisha na kuwawezesha wanawake.
Baadhi ya vikao muhimu vitaangazia mifumo ya kidijitali, ujasiriamali, na mifumo ya sera ambayo itaimarisha nafasi ya wanawake katika ngazi za uongozi.
Kwa viongozi vijana duniani na wajasiriamali wenye nia ya kufaidi masoko yanayoibuka, mkutano huu utakuwa ukiangazia fursa hizo pia.
Watoa mada wataonesha data za namna teknolojia inaweza kusaidia wanawake kuanzisha biashara na kuwa sehemu ya maendeleo ya uchumi.
Pia masuala kama ya haki za binadamu, upatikanaji sawa wa elimu kwa wote na namna sanaa na michezo inaweza kusaidia ukuzaji.
Watoa mada pia wataangazia namna hayo yote yatakavyoweza kusaidia kupazwa kwa sauti za wanawake kupitia tamaduni mbalimbali.