ULIMWENGU
2 dk kusoma
Kuachiliwa kwa mateka kutaanza Gaza saa 11 alfajiri, vyombo vya habari vya Israel vinaripoti
Hatua hiyo imekuja saa chache kabla ya mkutano wa kilele wa amani kuhusu usitishaji vita wa Gaza ambao utafanyika katika mji wa Sharm el-Sheikh nchini Misri.
Kuachiliwa kwa mateka kutaanza Gaza saa 11 alfajiri, vyombo vya habari vya Israel vinaripoti
Magari ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu yanaonekana Gaza [FILE]. / AA
13 Oktoba 2025

Kuachiliwa kwa mateka wa Kiyahudi waliokuwa wakishikiliwa Gaza kunatarajiwa kuanza saa 2 asubuhi (0500 GMT) kupitia njia ya Netzarim na kuendelea saa 4 asubuhi katika Khan Younis, Gaza, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti.

Waisraeli siku ya Jumatatu walijiandaa kuwapokea mateka 20 wa mwisho waliokuwa hai kutoka Gaza iliyoharibiwa, katika hatua muhimu ya kubadilishana mateka kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya miaka miwili ya vita vikali vya Tel Aviv dhidi ya ukanda wa Gaza wa Palestina.

Wapalestina nao walikuwa wakisubiri kuachiliwa kwa mamia ya watu waliokuwa wakishikiliwa na Israel.

Hatua hii ilikuja saa chache kabla ya mkutano wa amani kuhusu kusitisha mapigano Gaza, ambao utafanyika katika mji wa Sharm el-Sheikh nchini Misri, ukiongozwa kwa pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi.

Zaidi ya viongozi 20 wa dunia wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Mfalme Abdullah II wa Jordan, Mfalme Hamad bin Isa Al Khalifa wa Bahrain, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz.

Misri ilisema kuwa lengo la mkutano huo ni “kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza, kuimarisha juhudi za kuleta amani na utulivu katika Mashariki ya Kati, na kufungua hatua mpya ya usalama na utulivu wa kikanda.”

CHANZO:AA