Tuzo ya Nobel ya Amani 2025 ameshinda kiongozi wa upinzani wa Venezuela Maria Corina Machado, Kamati hiyo ya Norway ilitangaza siku ya Ijumaa.
Licha ya Rais wa Marekani Donald Trump kuiomba tuzo wazi hadharani, Machado, 58, alitunukiwa "kwa juhudi zake za kuimarisha haki za demokrasia kwa watu wa Venezuela."
Kulikuwa na wateule 338 kwa tuzo ya mwaka huu, ikiwemo watu 244 na mashirika 94.
Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka jana lilipewa shirika la Nihon Hidankyo, kundi la harakati za kuwasaidia walionusurika mabomu ya atomiki nchini Japan, “kwa juhudi zake za kupigania dunia isiyo na silaha za nyuklia kwa kutumia ushahidi wa watu kuwa silaha za nyuklia hazitakiwi kutumika tena.”
Kati ya 1901 na 2024, Tuzo ya Amani ya Nobel imetolewa mara 105 kwa washindi 142, ikiwemo watu 111 na mashirika 31.
Jumla ya mashirika 28 yamepata Tuzo ya Amani ya Nobel, huku shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu likipata tuzo hiyo mara tatu na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) likipokea mara mbili.
Tuzo za Nobel, zilizoanzishwa kulingana na wosia wa muasisi raia wa Uswidi Alfred Nobel na ya kwanza kutolewa 1901, zinaonekana kama baadhi ya tuzo zenye heshima kubwa duniani.
Hutolewa kila mwaka katika tasnia za fizikia, kemia, matibabu, fasihi, na amani, na baadaye ikaongezwa tuzo ya uchumi 1969 na Benki Kuu ya Uswidi.