ULIMWENGU
2 dk kusoma
Viongozi wa Marekani, Uturuki, Misri, na Qatar wamesaini makubaliano yanayositisha vita vya Gaza
Rais wa Marekani Trump anapongeza "siku kubwa kwa Mashariki ya Kati" wakati yeye na viongozi wa eneo hilo wakitia saini azimio la kusitisha mapigano Gaza baada ya mabadilishano ya wafungwa wa Israel na Hamas.
Viongozi wa Marekani, Uturuki, Misri, na Qatar wamesaini makubaliano yanayositisha vita vya Gaza
Uturuki, Misri, Qatar na Marekani zatia saini hati ya kusitisha mapigano Gaza. / / Reuters
13 Oktoba 2025

Misri, Qatar na Uturuki zimetia saini pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump hati ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza.

Hati hiyo ilisainiwa siku ya Jumatatu wakati wa mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Misri katika mji wa Sharm el-Sheikh.

Trump alipongeza "siku kubwa kwa Mashariki ya Kati" wakati yeye na viongozi wa eneo hilo walitia saini azimio lililokusudiwa kusisitiza usitishaji vita huko Gaza, saa chache baada ya Israel na Hamas kubadilishana mateka na wafungwa.

"Hii ni siku kubwa sana kwa ulimwengu, ni siku kubwa sana kwa Mashariki ya Kati," Trump alisema huku zaidi ya viongozi kumi na wawili wa dunia walikutana kuzungumza katika mkutano huo.

"Waraka huo utaelezea sheria na kanuni na mambo mengine mengi," Trump alisema kabla ya kutia saini, akirudia mara mbili kwamba "makubalioano ya kusitisha vita yatafanikiwa."

Mkutano wa ujenzi wa Gaza

Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi alisema kuwa nchi yake itaandaa mkutano kuhusu ujenzi mpya wa Gaza kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa na mateka.

"Misri itafanya kazi na Marekani kwa uratibu na washirika katika siku zijazo ili kuweka msingi wa ujenzi wa Gaza, na tunakusudia kuandaa mkutano wa mapema wa kufufua, kujenga na maendeleo," alisema.

Sisi pia alisema kuwa mkataba wa Gaza "unafunga wakati mgumu katika historia ya mwanadamu na kufungua enzi mpya ya amani na utulivu" kwa Mashariki ya Kati.

Aliongeza kuwa iliadhimisha "siku ya kihistoria" ya amani ambayo iliweka msingi wa suluhisho la serikali mbili.

CHANZO:TRT World