Rais wa Madagascar Andry Rajoelina hajulikani aliko, Waziri wa Usalama wa Umma Mandimbin'ny Aina Randriambelo ameliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumatatu, baada ya maandamano ya kutaka rais ajiuzulu kuungwa mkono na wanajeshi.
Rajoelina, ambaye hajaonekana hadharani tangu wiki iliyopita, anatarajiwa kuhutubia taifa Jumatatu jioni, ofisi yake ilisema mapema, baada ya kitengo kimoja cha jeshi kuungana na waandamanaji pamoja na kumteua mkuu mpya wa majeshi mwishoni mwa wiki.
Rajoelina, ambaye hajaonekena hadharani tangu Jumatano, alisema mwishoni mwa wiki kuwa kuna njama inaendelea "ya kuchukuwa madaraka kinyume cha sheria" katika taifa hilo.
Raia
Wakati huohuo, watu wameingia katika medani kubwa karibu na baraza la jiji la Antananarivo, wakipeperusha bendera, huku wakisubiri hotuba hiyo.
Maandamano hayo yaliyoanza Septemba kwanza yaliangazia kukatika kwa umeme na uhaba wa maji katika nchi hiyo na baadaye yakaendelea na kuwa harakati dhidi ya serikali wakitaka Rajoelina mwenye umri wa miaka 51 ajiuzulu.
Umoja wa Mataifa inasema watu wasiopungua 22 wameuawa katika siku za kwanza, na pia wahalifu wamepora mali.
Rajoelina amekanusha idadi hiyo, akisema wiki iliyopita "vifo 12 vilithibitishwa vya waporaji na waharibifu".