| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Tanzania yaingia hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza
Tanzania imefuzu katika hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu waliposhiriki kwa mara ya kwanza miaka 45 iliopita.
Tanzania yaingia hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza
Taifa Stars ya Tanzania. / Reuters
tokea masaa 12

Tanzania imemaliza katika nafasi ya tatu ya kundi B nyuma ya Nigeria na Tunisia. Walifungwa na Nigeria katika mechi ya kwanza lakini wakafanikiwa kutoka sare na Uganda na Tunisia. Licha ya kutoshinda mechi hata moja na kuwa na alama mbili pekee, watakabiliana na wenyeji Morocco katika hatua ya 16 bora baada ya kufuzu kama moja ya timu nne zilizomaliza vyema katika nafasi ya tatu.

Tanzania ilimaliza hatua ya makundi ikiwa na alama sawa na Angola, nafasi ya tatu katika kundi B, tofauti ikiwa kwenye magoli, wao wakiwa wamefunga goli moja zaidi.

Feisal Salum atakumbukwa kama shujaa wa taifa na mashabiki wa nchi hiyo baada ya kupiga shuti kali katika dakika ya 48 na kupata goli za kusawazisha dhidi ya Tunisia.

Hii ni hatua ya kihistoria kwa Tanzania ambao wanacheza kwenye mashindano hayo kwa mara ya nne sasa. Watakuwa wenyeji wa AFCON 2027 pamoja na Kenya na Uganda, kufanya michezo hiyo kupigwa Afrika mashariki kwa mara ya kwanza tangu yalipofanyika nchini Ethiopia 1976.

 

CHANZO:TRT Afrika Swahili