AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yashuka viwango vya ubora vya FIFA, Uganda yapanda
Kulingana na orodha hiyo iliyotolewa Septemba 18, 2025, Hispania imechupa hadi nafasi ya kwanza ikitokea ya pili, huku Argentina ikiporomoka hadi nafasi ya tatu kutokea ya pili.
Tanzania yashuka viwango vya ubora vya FIFA, Uganda yapanda
Baadhi ya wachezaji wa 'Taifa Stars'./Picha:@YoungAfricansEN
18 Septemba 2025

Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 103 hadi ya 107 kwa ubora wa soka duniani, kulingana na orodha ya viwango vya ubora iliyotolewa Septemba 18, 2025 na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Mabadiliko hayo yanatokana na matokeo ya hivi karibuni ya timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo ‘Taifa Stars’, katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.

‘Taifa Stars’ ilitoka sare ya 1-1 na Congo kabla ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Niger, katika michezo yake.

Wakati huo huo, Kenya imeanguka hadi nafasi ya 111 duniani kutoka ile ya awali ya 109, huku Uganda ikipanda kutoka 88 hadi 82 kwa ubora wa soka duniani.

DRC imepanda kwa nafasi moja, kutoka ya 61 hadi ya 60 katika orodha hiyo ya FIFA, wakati Burundi imedondoka kwa nafasi mbili kutoka 139 hadi 141.

Sudan Kusini ni ya 167 kwa ubora, Rwanda ya 127 wakati Somalia ikiwa katika nafasi ya 201.

CHANZO:TRT Afrika Swahili