Kesi ya uhaini inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar ilifunguliwa Jumatatu chini ya ulinzi mkali katika mji mkuu wa Juba, huku wakili wake akihoji kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Kuzuiliwa kwa Machar chini ya kifungo cha nyumbani tangu Machi kumezusha hofu ya kuzuka upya kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu 2013-2018 kati ya vikosi vyake vya kabila la Nuer na wapiganaji wa Dinka wanaomtii mpinzani wake wa muda mrefu Rais Salva Kiir.
Chama cha Machar cha SPLM-IO kinakataa mashtaka dhidi yake na wengine 20 ambayo ni pamoja na mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa madai ya kuhusika katika uvamizi wa wanamgambo wa Jeshi la White Army wanaotawaliwa na Nuer kaskazini mashariki mapema mwaka huu.
Katika mahakama maalum, Machar alionekana hadharani tangu kuzuiliwa kwake nyumbani mwezi machi 2025.
Kiir alimsimamisha kazi kwa amri mapema mwezi huu huku mashtaka yakifichuliwa.
Shirika la utangazaji la serikali ndilo liliruhusiwa pekee kufanya matangazo ya mahakamani.
Geri Raimondo Legge, wakili wa Machar, alisema kuwa mahakama hiyo "ilikuwa kinyume cha sheria na batili" kwa sababu, alisema, Machar alikuwa na kinga kwa kuwa Makamu wa Rais anayehudumu.
Washirika saba wa Machar walishtakiwa pamoja naye mapema mwezi huu, akiwemo waziri wa nishati.
"Tunaomba mahakama iamuru kuachiliwa mara moja kwa Mheshimiwa Dkt Riek Machar Teny, Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, na washtakiwa saba kwa kukamatwa na kuzuiliwa kinyume na katiba," Legge aliiambia mahakama.
Mwendesha mashtaka Ajo Ony'Ohisa Igele alizitaja hoja za upande wa utetezi kuwa "zisizo na msingi na dhaifu."
Serikali inamtuhumu Machar kwa kuunga mkono Jeshi la White Army, wanamgambo wa kabila ambalo kwa kiasi kikubwa lina vijana wa Nuer, wakati wa mapigano na jeshi katika mji wa kaskazini mashariki wa Nasir mwezi Machi.
Raia kadhaa waliuawa na zaidi ya watu 80,000 kukimbia makazi yao.
Kiir na Machar, wote wakiwa na umri wa miaka 70, walihudumu katika serikali ya umoja iliyo dhaifu kama sehemu ya makubaliano ya amani ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kiongozi wa zamani wa waasi, Machar amekuwa na uhusiano mbaya na Rais Kiir kwa zaidi ya miongo mitatu.