AFRIKA
1 dk kusoma
Salum Mwalim wa CHAUMMA aahidi kupambana na ukosefu wa ajira Tanzania
Watanzania wataingia kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Salum Mwalim wa CHAUMMA aahidi kupambana na ukosefu wa ajira Tanzania
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHAUMMA, Salum Mwalim./Picha:@ChaummaT
19 Septemba 2025

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Salum Mwalim amesema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira nchini humo, litakuwa historia endapo atachaguliwa kuiongoza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza Septemba 19, 2025 katika kata ya Nyakanazi Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera, akiwa njiani kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya kampeni zake, Mwalim amewahakikishia Watanzania juu ya uwepo wa kwa uchumi jumuishi katika sekta na kada mbalimbali, ili kuweza kondoa tatizo la ajira nchini humo.

Mgombea huyo aliongeza kuwa, kupitia sera yake ya kilimo, atahakikisha mazao ya kimkakati kama vile kahawa na pamba, yanatengenezewa mazingira bora ya kuzalishwa na kupatikana kwa masoko ya uhakika yatayokuwa yananufaisha wananchi na si kuwadidimiza.

Watanzania wataingia kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Mchakato huo umepewa uzito wa kipekee, hasa kweye kipimo cha imani ya wananchi katika mfumo wa kidemokrasia.

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), kuna jumla ya vyama vya siasa 18 ambavyo zinashiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.

CHANZO:TRT Afrika Swahili