Tangazo hilo limetolewa kupitia Notisi ya Kisheria No. 157 iliyochapishwa kwenye Kiambatisho cha Gazeti Rasmi la Serikali la Kenya tarehe 19 Septemba 2025, likitolewa na Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, chini ya Kifungu cha 3(3) cha sheria hiyo.
Agizo hilo, linalojulikana kama Agizo la Kuzuia Ugaidi, 2025, linaanza kutumika mara moja na litaendelea kuwa hivyo hadi pale litakapotenguliwa na Waziri au Mahakama.
Agizo hilo linafanya kuwa kosa la jinai kuwa mwanachama, kuunga mkono, kuchangisha fedha, au kueneza propaganda inayohusiana na mashirika hayo.
Kifungu cha 3(3) cha sheria hiyo kinairuhusu serikali, kufunga mali za mashirika hayo, kupiga marufuku mikutano yao, na kufungua mashtaka dhidi ya mtu yeyote anayehusiana na makundi hayo.
Kwa hatua hii, Kenya inajiunga na nchi kama Misri, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), na Bahrain, ambazo tayari zimetangaza rasmi Muslim Brotherhood kuwa shirika la kigaidi.
Kundi la Muslim Brotherhood lilianzishwa nchini Misri mwaka 1928, na linachukuliwa kuwa chanzo kikuu cha kifikra cha Uislamu wa kisiasa wa kisasa, likiwa na matawi mbalimbali katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.