Na Tunç Demirtaş
Kinachotokea wakayi huu el-Fasher, kwa njia nyingi, ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kuna ushahidi wa kutosha kuonesha kuwa RSF imehusika na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Ndani ya wiki moja, maelfu ya watu wameuawa kikatili dunia ikitizama. Kwa vyovyote vile, hili ni janga kwa watu.
Na hii siyo mara ya kwanza kwa Sudan kupitia matatizo haya. Kwa miezi kumi na nane iliopita, watu wa el-Fasher tayari wamekuwa katika hali mbaya, wanakufa polepole. Hawakuwa wanapata chakula.
Wakati fulani, walilazimika kula chakula cha wanyama hadi nyama ya tumbili, panya, na paka.
Kuanguka kwa mfumo wa haki duniani na msimamo wa Uturuki wa aina yake
Uturuki, pamoja na mataifa kadhaa, imeanza kuzungumzia suala la kuunga mkono watu wa Sudan dhidi ya ukatili wa RSF. Hili linaashiria mtazamo wa Uturuki wa kuzingatia utu kama sehemu ya sera yake ya mambo ya nje. Kote kwa matatizo yanayokumba kuanzia Sudan hadi Gaza sauti ya Uturuki imekuwa ikiskika kila mara na imekuwa na ujasiri na kutoa muelekeo wa wazi.
Itambulike kuwa Rais Recep Tayyip Erdoğan ni mmoja kati ya viongozi wachache duniani ambayo wameleta suala la madhila ya watu wa Sudan katika mjadala wa kimataifa.
Kwa bahati mbaya, wengine wachache wamefanya hivyo pia. Umoja wa Mataifa, wakati huohuo, imeshindwa kuwajibika ipasavyo. Swali siyo kama jamii ya kimataifa inaweza kuingilia kati, lakini kama inataka kufanya hivyo.
Muenendo wa sasa hautoi tena suluhu au kutekeleza haki. Ilionekana Gaza, na kabla ya hapo Bosnia na Rwanda. Sasa, inafanyika Sudan.
Hakuna hatua ya kuwafanya waliotekeleza ukatili. Kila tukio chanzo chake ni ukosefu wa maadili na mfumo wa dunia wa sasa unaoendekeza mfumo huo hasa.
Umuhimu wa kimkakati wa El-Fasher na masuala ya kujifunza ambayo hayakuzingatiwa
El-Fasher ni mji muhimu wa kimkakati. Ukiangalia ramani utagundua kuwa ni eneo la biashara nyingi, hasa wakati wa vita. Ukiweza kudhibiti njia hizi inamaanisha unaweza kudhibiti njia ya bidhaa.
Ni muhimu kutambua kuwa, eneo lenye utajiri mkubwa wa dhahabu la liko sehemu ya Jebel Amir na Songo. Umuhimu wa El-Fasher siyo kwa ajili ya raslimali zake lakini kwa nafasi yake ya kuunganisha mashariki na magharibi mwa Sudan. Pia ina uwanja wa ndege ambao una umuhimu katika masuala ya operesheni.
Darfur ina miji mikubwa mitano. El-Fasher ndiyo mji mkuu Darfur Kaskazini. Hadi wiki iliopita, mji wa Darfur ulikuwa chini ya udhibiti wa jeshi huku wapiganaji wa RSF tayari walikuwa wanadhibiti maeneo ya Kusini, Magharibi, Kati, na Darfur Mashariki.
Baada ya kushambulia watu wa Darfur kwa mwaka mmoja na nusu, RSF sasa imechukuwa udhibiti wa mji wa el-Fasher, na kufanya Darfur nzima kuwa chini ya udhibiti wao.
Wakati huohuo kinachoendelea El-Fasher ni mauaji ya kimbari. Kuna sheria za vita lakini wapiganaji wa RSF hawazizingatii zote.
Picha za satelaiti zinaonesha makaburi ya halaiki na mauaji kila mahali. Ili kukomesha ukatili zaidi na kulinda haki za binadamu kunatakiwa kupawe kipaumbele duniani.
Kwa hiyo, dalili zote zinaonesha kuwa RSF itaendelea kukiuka sheria za haki za binadamu za kimataifa na utaratibu kwa binadamu.
Taarifa zinaonesha kuwa, kwa mfano, kiongozi wa wapiganaji anayejulikana kama “Abu Lulu” yeye mwenyewe amewaua na kuagiza kuuawa kwa raia wengi. Haya ni moja ya matukio mengi. Suala kuu hapa ni kuwa hakuna vikwazo vya uhakika.
Mwandishi, Tunç Demirtaş ni mhadhiri katika idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Mersin, Uturuki
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.






















