| swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Maafisa 2 wa Kenya wamefariki baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa na kundi la al-Shabab
Maafisa wawili wa Kikosi cha Ulinzi wa Mipakani nchini Kenya wamefariki siku ya Jumatano baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa ardhini (IED) na wanamgambo wa al-Shabab wanaotoka Somalia, kwa mujibu wa polisi wa Kenya.
Maafisa 2 wa Kenya wamefariki baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa na kundi la al-Shabab
Mamlaka za Kenya zinasema al-Shabab bado ni tishio kubwa, hususan kupitia mabomu ya kutegwa ardhini. /
tokea masaa 15

Shambulio hilo lilitokea karibu na mpaka wa Kenya na Somalia katika Kaunti ya Garissa, eneo lililo takriban kilomita 370 kaskazini mashariki mwa mji mkuu, Nairobi.

Maafisa wa polisi waliozungumza na wanahabari walisema wanachama wa al-Shabab walitega na kulipua kifaa hicho wakati maafisa hao wakiwa doria, na kuliharibu kabisa gari lao na kuwaua papo hapo.

Vikosi vya usalama vimetumwa kulidhibiti eneo hilo, ambako kundi hilo la wapiganaji limekuwa likiwalenga mara kwa mara maafisa wa usalama na kuvuruga shughuli za ulinzi mpakani.

Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha gari la doria lililosambaratika na kupinduka upande mmoja, vipande vya chuma vilivyosambaa barabarani, na shimo kubwa linaloaminika kuwa sehemu ya mlipuko; maafisa pia walionekana wakichunguza mabaki hayo.

Kenya imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na al-Shabab tangu ilipotuma wanajeshi Somalia mwaka 2011 chini ya Kikosi cha Umoja wa Afrika (sasa ATMIS).

Kundi hilo la kigaidi mara nyingi hufanya mashambulizi ya kuvizia mpakani, kulipua mabomu barabarani hasa yakilenga doria za polisi, na kushambulia vituo vya polisi vilivyo maeneo ya ndani, kwa lengo la kuishinikiza Kenya iondoe wanajeshi wake Somalia.

Kaunti za Garissa, Mandera na Wajir, zinazopakana na Somalia ndizo zimeathiriwa zaidi, huku al-Shabab wakitumia mianya katika mipaka, miundombinu duni ya barabara na mazingira ya mbali ili kufanya mashambulizi.

Licha ya doria kuongezwa na uangalizi kuimarishwa, mamlaka za Kenya zinasema al-Shabab bado ni tishio kubwa, hususan kupitia mabomu ya kutegwa ardhini (IED), ambayo yameua makumi ya maafisa wa usalama katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Bassirou Diomaye Faye: Rais wa Senegal
Wataalamu wa Afrika watoa wito wa kukaguliwa tathmini ya viwango vya mikopo kwa bara
Eswatini yapokea dola milioni 5.1 kupokea wahamiaji waliofurushwa Marekani, waziri anasema
Gabon yatia saini makubaliano ya kihistoria ya ufadhili wa hali ya hewa kwa misitu ya mvua ya Congo
Wanajeshi wa RSF wameripotiwa kupata hasara kubwa katika jimbo la Kordofan Kaskazini nchini Sudan
CAF yatangaza wasimamizi maarufu wa sherehe ya Tuzo za CAF 2025
Jeshi la Somalia limewauwa magaidi 11 wa Al Shabab na kuzuia shambulio la kujitoa muhanga
Tanzania huenda ikakabiliwa na changamoto kupata mikopo kutoka nje, amesema Rais Samia
Sura mpya Baraza la Mawaziri Tanzania
Cape Verde, Mauritius na Ushelisheli wafanikiwa kuangamiza surua na  rubela
Rais wa Sudan Kusini Kiir amrejesha makamu wa rais katika mabadiliko ya baraza la mawaziri
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao kutoka Al Fasher ya Sudan tangu kutwaliwa na RSF
Rais wa Tanzania amteua binti na mkwe wake katika Baraza la Mawaziri
Rais Samia amteua waziri mpya wa fedha, awaacha mawaziri wa mambo ya nje na madini madarakani
Tovuti za taasisi za serikali ya Kenya zashambuliwa
Mgodi waporomoka DRC na kuua watu wasiopungua 32
Wahamiaji 4 wafariki baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba makumi ya watu kuzama pwani ya Libya
Kikundi cha matabibu kinaripoti visa ya ubakaji wa wasichana wa Al Fasher baada ya RSF kuteka
Mlipuko wa virusi vya Marburg umethibitishwa kusini mwa Ethiopia
DR Congo, M23 wasaini makubaliano ya amani 'ya kihistoria' nchini Qatar