CAF yatangaza wasimamizi maarufu wa sherehe ya Tuzo za CAF 2025
AFRIKA
3 dk kusoma
CAF yatangaza wasimamizi maarufu wa sherehe ya Tuzo za CAF 2025CAF imesema itawaleta pamoja mwimbaji aliyeshinda tuzo za Grammy Angélique Kidjo na mcheshi wa Morocco Tahar Lazrak ili kuakisi kikamilifu utofauti wa kisanii na ufikiaji wa kitamaduni wa bara.
Angélique Kidjo ametoa zaidi ya nyimbo 180.
tokea masaa 7

Shirika la Soka Afrika (CAF) limetangaza wasimamizi wa sherehe ya Tuzo za CAF 2025, itakayofanyika tarehe 19 Novemba katika Chuo Kikuu cha Polytechnique Mohammed VI, Rabat.

Nyota wa muziki mwenye tuzo nyingi za Grammy, Angélique Kidjo, pamoja na mwigizaji na mcheshi maarufu kutoka Morocco, Tahar Lazrak anayejulikana kwa jina la Oualas, ndio watakaokuwa waandalizi wa usiku huo wa kipekee unaosherehesha wachezaji na maafisa bora wa soka barani Afrika.

CAF imesema wawili hao hao wamechaguliwa kwa makini kuakisi utofauti wa sanaa na ushawishi wa kitamaduni unaotambulisha ubunifu wa kisasa wa Kiafrika.

“ Tukiwa pamoja, na kuchaguliwa kwa wawili hao inathibitisha azma ya CAF ya kuandaa sherehe inayosherehekea si tu mafanikio ya michezo, bali pia vipaji vya kitamaduni vya Afrika,” CAF ilisema kwenye taarifa yake.

Nyota wa muziki wa kimataifa

Kwa Kidjo, kuongoza sherehe hii ni sura nyingine katika maisha yake ya kipekee. Kama balozi wa ubunifu wa Kiafrika duniani, nyota huyu wa Benini amekuwa akibadilisha upya muziki wa dunia kwa zaidi ya muongo tatu, akichanganya muziki wa ulimwengu na midundo ya Kiafrika.

Akiwa na tuzo 5 za Grammy, albamu 16, na nyimbo zaidi ya 180, Kidjo ameitumikia tamasha kubwa zaidi duniani na kushirikiana na wasanii kama Alicia Keys, John Legend, na Burna Boy.

Mchango wake unapanuka zaidi ya jukwaa la muziki; alipewa heshima ya kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi wa Time Magazine mwaka 2021. Pia ni Balozi wa UNICEF wa Haki za Binadamu na mchapakazi wa haki za wanawake, elimu, na utunzaji wa urithi wa kitamaduni wa Afrika.

Nyota anayeinuka kutoka Morocco

Kutana na Oualas, mcheshi, mwigizaji, na mwandalizi wa onyesho aliyejipatia umaarufu mkubwa nchini Morocco na barani Afrika, akifahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kuigiza kama mchekeshaji.

Oualas anajulikana kwa ucheshi wake wa kubuni na mtindo wa vicheko unaogusa vizazi mbalimbali, jambo lilimfanya kuwa miongoni mwa wasanii wapendwa zaidi Kaskazini mwa Afrika.

“Oualas ataongeza joto, nguvu, na haiba katika usiku huu utakao wakumbuka walio bora katika soka barani Afrika,” CAF ilisema.

Hafla ya Tuzo za CAF 2025 itatoa baadhi ya tuzo za heshima zikitolewa kwa wachezaji na maafisa wakuu wa mpira wa miguu. Hizi ni pamoja na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Wanaume na Wanawake.

Pia kutakuwa na Tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka, Mchezaji Bora wa Mwaka wa mashindano ya Klabu za Afrika kuwatambua wachezaji bora katika mashindano ya vilabu barani Afrika, na Kocha Bora.

Wachezaji wapya wenye pia kutambuliwa kupitia tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka, huku tuzo za Timu ya Taifa ya Mwaka na Klabu Bora ya Mwaka zikiangazia nguvu ya pamoja katika ngazi za kitaifa na klabu.

Soma zaidi
Rais wa Sudan Kusini Kiir amrejesha makamu wa rais katika mabadiliko ya baraza la mawaziri
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao kutoka Al Fasher ya Sudan tangu kutwaliwa na RSF
Rais wa Tanzania amteua binti na mkwe wake katika Baraza la Mawaziri
Rais Samia amteua waziri mpya wa fedha, awaacha mawaziri wa mambo ya nje na madini madarakani
Tovuti za taasisi za serikali ya Kenya zashambuliwa
Mgodi waporomoka DRC na kuua watu wasiopungua 32
Wahamiaji 4 wafariki baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba makumi ya watu kuzama pwani ya Libya
Kikundi cha matabibu kinaripoti visa ya ubakaji wa wasichana wa Al Fasher baada ya RSF kuteka
Mlipuko wa virusi vya Marburg umethibitishwa kusini mwa Ethiopia
DR Congo, M23 wasaini makubaliano ya amani 'ya kihistoria' nchini Qatar
Baraza la Maaskofu Tanzania lataka uwajibikaji kwa waliohusika na mauaji ya waandamanaji
Baraza la usalama la UN laongezea mwaka mmoja ujumbe wa amani wa Abyei
Kiongozi wa zamani wa waasi wa DRC anayeshtakiwa Paris kwa uhalifu wa kivita aanza mgomo wa kula
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi