UTURUKI
1 dk kusoma
Maonesho ya teknolojia ya Uturuki ya TEKNOFEST yaanza jijini Istanbul
Onesho hilo kubwa la mambo ya anga na teknolojia, huvutia mamia kwa maelfu ya watu kila mwaka.
Maonesho ya teknolojia ya Uturuki ya TEKNOFEST yaanza jijini Istanbul
Onesho la TEKNOFEST. / AA
17 Septemba 2025

Maonesho makubwa ya teknolojia, maarufu kama TEKNOFEST yameanza rasmi siku ya Jumatano, jijini Istanbul nchini Uturuki.

Tukio hilo la siku tano ambalo linafanyika kwenye uwanja wa ndege wa Ataturk, linaandaliwa na Timu ya Teknolojia ya Uturuki (T3) pamoja na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya nchini Uturuki.

Onesho hilo lilianza kufanyika kuanzia mwaka 2018 kwa msaada wa taasisi mbalimbali za serikali, sekta binafsi na vyuo vikuu.

Hadi kufikia sasa, onesho hilo limeshirikisha matukio makuu 58 yenye vipengele 137.

Kupitia onesho hilo, washiriki kutoka pande zote za dunia huwezi kushirikishana elimu na uzoefu kwenye sekta ya nyanja ya maendeleo kiteknolojia.

Teknolojia, furaha

Onesho la linawakaribisha wageni hadi siku ya Jumapili sio kwa mashindano tu, bali na matukio mengine ya kuvutia.

Tukio hilo huhusisha maonesho mbalimbali ya kuvutia kama vile ya kurusha ndege, warsha na masuala mbalimbali ya kiiteknolojia.

Onesho hilo limekuwa likifanyika katika miji mbalimbali nchini Uturuki.

Kwa nyakati tofauti, onesho hilo limewahi kufanyika nchini Azerbaijan na katika Jamhuri ya Uturuki ya Kaskazini mwa Cyprus.

Mwezi uliopita, onesho lililopewa jian la Blue Homeland, lenye dhima ya usafiri wa maji lilifanyika jijini Istanbul.

 

CHANZO:TRT World