UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan alaani "ugaidi wa kiserikali" wa Israel na kuahidi kuendelea kuiunga mkono Palestina
Uchokozi wa Israel unalenga mataifa yote ya Kiislamu, sio Palestina pekee, anaonya Erdogan, akitaka "hatua zote madhubuti zinazowezekana na kisheria" kukomesha kutojali kwake.
Erdogan alaani "ugaidi wa kiserikali" wa Israel na kuahidi kuendelea kuiunga mkono Palestina
Erdogan alipongezwa kupitishwa Azimio la New York na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hivi karibuni kwa kura 142. / / AA
16 Septemba 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema shambulio la Israel dhidi ya kundi la wasuluhishi mjini Doha lilikuwa "shambulio la woga" lililotoa "changamoto ya wazi kwa mfumo na sheria za kimataifa," baada ya kufanya mashambulizi Gaza, Syria, Lebanon, Yemen na Iran.

"Shambulio hili kwa mara nyingine limeonyesha ukubwa wa fikra za uvamizi wa Israel na sera za kigaidi," Erdogan aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne aliporejea kutoka katika mkutano wa dharura wa nchi za Kiarabu na Kiislamu mjini Doha.

Rais alisisitiza kuwa Uturuki ilisimama kidete pamoja na Qatar na watu wa Palestina, akitoa salamu za rambirambi kwa waliouawa na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Ameongeza kuwa mkutano huo wa dharura umedhihirisha msimamo wa umoja wa ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya uvamizi wa Israel, huku viongozi wakikubali kuzingatia hatua za ziada za kidiplomasia na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupitia upya uhusiano na Tel Aviv.

Kuhusiana na taarifa ya pamoja , alibainisha, ilisisitiza kuwa uchokozi wa Israel haujalenga Palestina pekee bali mataifa yote ya Kiislamu, na kutaka kupitishwa kwa "hatua zote madhubuti zinazowezekana na kisheria " kusitisha vitendo vyake.

Erdogan alipongeza kupitishwa kwa Azimio la New York na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hivi karibuni kwa kura 142, na kuelezea kama hatua ya mabadiliko katika juhudi za kidiplomasia kwa suluhisho la mataifa mawili.

"Inathibitisha kuwa Israel inazidi kutengwa na kwamba msimamo wa Uturuki umepata kutambuliwa kimataifa," alisema.

"Madai ya uwongo"

Akizungumzia mvutano wa kikanda, Erdogan alikataa "madai ya uwongo" ya kuchora upya mipaka kwa kisingizio cha "nchi ya ahadi."

Madai kama hayo, alisema, yalikuwa batili kisheria na yamefilisika kimaadili, yakitumikia tu ajenda ya "itikadi kali na ya kifashisti" ya Israel.

Pia alisema kuwa uongozi wa Israel umebadilisha itikadi kali na kuwa "mtandao wa kifashisti wa mauaji" ambao unaleta tishio kwa Waislamu, Wakristo na Wayahudi vile vile. Ameyataka mataifa ya Kiislamu kujibu kwa ujuzi, ushirikiano na umoja.

"Unapowasikiliza Wayahudi wanaopinga mauaji ya halaiki ya Israel, unaweza kuona wazi jinsi itikadi ya Uzayuni ilivyo hatari. Ikiwa Israel ya Kizayuni itahusishwa na chochote, ni ugaidi na ufashisti."

Rais alisisitiza tena kwamba Ankara itaendelea kuwa kama "bendera ya Palestina", akisisitiza kwamba lengo kuu la Uturuki lilikuwa kuhakikisha amani, haki na utu wa binadamu katika eneo lote.

CHANZO:TRT World