UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan:Uturuki ipo pamoja na wale wanaolengwa na ‘uhalifu wa Israel’
Rais wa Uturuki amesema kuwa hakuna atakayeizuia Ankara kusimama pamoja na watu wa Gaza wanaoonewa chini ya mashambulizi ya Israel.
Erdogan:Uturuki ipo pamoja na wale wanaolengwa na ‘uhalifu wa Israel’
Rais Erdogan wa Uturuki./Picha:AA
17 Septemba 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa hutoba nzito, akiahidi kuendelea kuwasaidia Wapalestina na kulaani mashambulizi ya Israel huko Gaza.

"Hatutoruhusu Yerusalemu ichafuliwe na mikono michafu, ingawa najua kuwa nia ya wapenzi wa Hitler haitoisha," alisema Rais Erdogan siku ya Jumatano wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki jijini Ankara.

Rais Erdogan aliapa kuwa Waislamu “hawatorudi nyuma kuhusiana na haki zao za Yerusalemu.”

Alisema Rais wa Uturuki, "Wale ambao wanaamini wana uwezo wa kujenga kesho iliyo salama hyuku kukiwa na ukandamizaji na mauaji ya kimbari ya watoto wasio na hatia watazama kwenye damu waliyoimwaga."

Kulingana na Erdogan, Uturuki itaendelea “kusimama pamoja na wale wote wanaolengwa na uhalifu wa Israel, kuanzia Syria hadi Yemen, Lebanon mpaka Qatar”, na kuonesha uyatari wa Ankara kuisaidia Gaza.

CHANZO:TRT World and Agencies