Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameitaka jumuiya ya Kiislamu duniani kuiongezea Israel shinikizo, akisema kuwa hatua za kiuchumi zitumike kuidhibiti Tel Aviv.
"Ni lazima kuongeza jitihada zetu za kidiplomasia na kuongeza vikwazo dhidi ya Israel," alisema Erdogan, akionya kuwa serikali ya Netanyahu inalenga "kuongeza mauaji ya kimbari huko Palestina na kuchochea mapigano katika kanda ".
Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja Waarabu na Waislamu jijini Doha siku ya Jumatatu, rais huyo wa Uturuki alisisitiza kuwa mataifa ya Kiislamu, yana “uwezo na sababu” ya kukabiliana na utanuzi wa Israel ", na kulaani hulka ya Kiisrael, aliyoiita ya “unywaji damu na zitokanazo na vurugu”.
"Uturuki ipo tayari kushirikisha uwezi wake katika sekta la ulinzi na nchi za marafiki," alisema Rais Erdogan.
"Ni lazima tuongeze ushirikiano wetu kwa karne zijazo."