Jiji la Istanbul ni mwenyeji wa kuimarika kwa ushirikiano na Afrika - Jukwaa la 5 la Uturuki na Afrika la Biashara na Uchumi, linalojulikana kama TABEF 2025.
Mkutano huo wa siku mbili chini ya mada ya “kuimarisha Uhusiano wa Uturuki na Afrika kwa Manufaa ya Wote,” unafanyika kuanzia Jumatano katika Ukumbi wa Mikutano wa Istanbul na kuleta pamoja viongozi wa biashara, wawekezaji, watungasera na wajasiriamali 4,000 kutoka barani Afrika.
Lakini jukwaa hilo ni zaidi ya siku mbili za mkutano, linawakilisha miongo miwili ya diplomasia, maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi.
Ushirikiano wa Uturuki na Afrika uliimarika 2008, wakati wa Kongamano la kwanza la Uturuki na Afrika lilipofanyika jijini Istanbul. Huku kukiwa na nchi 49 za Afrika zikishiriki na mashirika 11 ya kimataifa, yalikuja na nyaraka mbili muhimu: Azimio la Istanbul na Mfumo wa Ushirikiano, na kuweka msingi wa ushirikiano wa muda mrefu.
Tangu wakati huo, sera ya Uturuki na Afrika imebadilika—katika kufungua mradi wa Afrika uliozinduliwa 1998, hadi kwenye Sera ya Ushirikiano wa Afrika 2013.
Na matokeo yako wazi.
2003, biashara kati ya Uturuki na Afrika ikiwa ni dila bilioni 5.4.
Kufikia mwisho wa 2022, ilikuwa imefika dola bilioni 40.7. 2024, biashatra ilikuwa dola bilioni 36.5, huku kuuza nje ya nchi ikiwa ni dola bilioni 21.8 na bidhaa za kuingizwa nchini dola bilioni 15.
Na mwaka huur? Katika kipindi cha miezi minane ya 2025, Uturuki iliuza bidhaa barani Afrika za dola bilioni 14.6 na kuingiza bidhaa za dola bilioni 7.7, na kufanya kiwango kuwa dola bilioni 22.3. Kulingana na Rais wa DEİK Nail Olpak, biashara inatarajiwa kuongezeka zaidi ya dola bilioni 35 kufikia mwisho wa mwaka.
Washirika wakuu katika biashara ni Misri, Algeria, Libya, Afrika Kusini, na Nigeria. Lakini lengo la Uturuki ni pana—kufikia nchi nyingi za Jangwa la Sahara na kuendeleza biashara kwa mataifa mengi zaidi.
Baadhi ya bidhaa zinazouzwa nje kwa wingi ni mashine, vyuma, bidhaa za nishati, bidhaa za umeme, plastiki, na vyakula—hasa unga na mafuta. Bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zinaangazia nishati, kakao, kilimo, na madini.
Nail Olpak anasisitiza umuhimu wa kuangazia soko la Afrika, ikiwemo mipango ya usafiri, ufikiwaji wa fedha, na Makubaliano mapya ya Biashara Huru.
Tayari, Uturuki ina makubaliano ya Biashara Huru (FTA) na Misri, Tunisia, Morocco, na Mauritius. Makubaliano na Sudan, Ghana, Cameroon, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yako katika hatua ya majadiliano.
Kwa uhalisia, Uturuki inawekeza —siyo tu kwa biashara.
Uwekezaji wake wa moja kwa moja umepita dola bilioni 10. Wajenzi wa Uturuki wamekamilisha miradi zaidi ya 2,000, wenye yenye gharama ya doola bilioni 97 —kutoka viwanja vya ndege na barabara hadi hospitali na ujenzi wa nyumba.
Na yote imeunganishwa. Shirika la ndege la Turkish Airlines sasa inasafiri hadi katika mataifa 51 nchi za Afrika zikiwa 39. Uturuki pia una balozi 44 kote barani Afrika —kutoka balozi 12 mwaka 2002.
Ongeza kwa hilo kazi ya shirika la TİKA, Wakfu wa Maarif, na Taasisi ya Yunus Emre, na hivyo picha inakuwa wazi: Uturuki haijengi tu njia za biashara, lakini pia kujenga uaminifu na miunganisho ya watu.
Jukwaa la TABEF mwaka huu limeweka mkazo katika kilimo na usalama wa chakula, nishati ya kijani na mbadala, madini na maliasili, vifaa na usafiri, teknolojia ya kidijitali, ujenzi na miundombinu, ulinzi na tasnia ya hali ya juu.
Mikutano kati ya wafanyabiashara (B2B) na kati ya serikali na wafanyabiashara (G2B) ilifanyika pamoja na mijadala ya jopo na vikao vya mikutano, ikitoa fursa adimu ya mashirikiano ya ana kwa ana kati ya wadau wa Kiafrika na Kituruki.
Kwa hiyo, Uturuki na Afrika zinaweka malengo makubwa: dola bilioni 40 katika biashara ifikapo 2026, dola bilioni 50 muda mfupi baadaye na maono ya ujasiri ya dola bilioni 75 katika miaka ijayo.