UTURUKI
3 dk kusoma
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan atetea nafasi ya wanawake katika Jukwaa la Uturuki-Afrika
Katika hotuba yake kwenye Jukwaa la Tano la Biashara na Uchumi la Uturuki-Afrika siku ya Alhamisi, Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan alisisitiza nafasi muhimu ya wanawake katika kuunda simulizi mpya ya kimataifa.
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan atetea nafasi ya wanawake katika Jukwaa la Uturuki-Afrika
Mke wa Rais wa Uturuki, Emine Erdogan alieleza kuwa hisia ya mwanamke inapochanganywa na uongozi, huibua suluhisho kwa utu wa binadamu na mazingira. / / AA
16 Oktoba 2025

Mke wa Rais Emine Erdogan alisisitiza kuwa vita, mauaji ya halaiki, mabadiliko ya tabianchi na umasikini bado vinaendelea kuwa masuala ya msingi katika ajenda ya dunia.

"Hakika, dunia inahitaji simulizi mpya,” Bi Erdogan alisema.

“Ninaamini kuwa simulizi hiyo itaandikwa kwa kalamu ya mwanamke. Kila siku, katika kona tofauti ya dunia, mwanamke mmoja anageuza wazo kuwa uhalisia. Kama vile maua yanavyochipuka katikati ya theluji, mawazo haya yanatia matumaini kwa binadamu hata katika mazingira magumu kabisa.”

Akiangazia sifa za uongozi za wanawake, alibainisha kuwa wanawake sio tu hutoa suluhu kwa matatizo ya kimataifa lakini pia wanakuza utamaduni wa amani.

“Vizazi vilotokana mikononi mwa wanawake hufanikiwa kuunda mustakabali mzuri. Hivyo basi, wanawake wanaposhiriki katika maisha ya kiuchumi, hawajiendelezi wao tu bali pia jamii zao."

Ushirikiano wa uchumi katia ya Uturuki na Afrika

Mke wa Rais Emine Erdogan alisisitiza zaidi ushirikiani kati ya Uturuki na Afrika, akielezea kanda hizo mbili kama wadau muhimu katika uchumi wa dunia.

Hisia ya mwanamke inapochanganywa na uongozi, huibua suluhisho jumuishi linalolinda utu wa binadamu pamoja na mazingira. Dunia inahitaji mkono wa mwanamke katika kila janga la kimataifa, kimazingira na kibinadamu.” Mke wa Rais Emine Erdogan alisisitiza ndiyo maana ninaamini kwa dhati kwamba wanawake wanapaswa kuwa katika nafasi ya msingi katika uhusiano kati ya Uturuki na nchi za Afrika.

Akitaja mara kadhaa alivyotembelea nchi za Afrika kufuatia mpango wa Uturuki kwa Afrika ulioanzishwa mwaka 2005, Mkw wa Rais Eimne Erdogan aliongeza: "Nilipata fursa ya kuzitembelea nchi 30 tofauti. Mara nyingi nilishuhudia kwa macho yangu nguvu ya wanawake wa Kiafrika, busara na bidii yao pamoja na mchango wao kwa jamii zao. Tangu mwanzo, nimekuwa na hamu kubwa ya kushirikiana na wanawake hawa jasiri."

Alielezea matumaini kuhusu siku zijazo, akitoa mfano wa idadi ya vijana na mifumo ya ujasiriamali yenye nguvu ya Uturuki na Afrika.

"Uturuki na Afrika ni maeneo mawili ambayo yanasimama vyema katika uchumi wa dunia. Ninaamini wanawake, ikiwa wataungwa mkono vya kutosha, watafanya nchi zetu kuwa nyota zinazong'aa katika karne ya 21."

Kupitia chapisho la mitandao ya kijamii baada ya jukwaa hilo, Mkw wa Rais Emine Erdogan alisema: "Mwaka huu, nilipata heshima ya kukutana na wawakilishi mashuhuri kutoka sekta ya biashara na jumuiya za kiraia katika kikao cha mahojiano kuhusu 'Uongozi wa Wanawake na Ujasiriamali', iliyoandaliwa kama sehemu ya Jukwaa la Tano la Biashara na Uchumi kati ya Uturuki na Afrika. Tulijadili sera zitakazoongeza mchango wa wanawake katika maendeleo ya kiuchumi ya Uturuki na Afrika. Ushirikiano unaozidi kuimarika kati ya nchi yetu na mataifa ya Afrika unaelekea kwenye mustakabali jumuishi, wenye tija na tumaini chini ya uongozi wa wanawake."

"Afrika imekuwa na nafasi maalum siku zote katika moyo wangu"

Pia alithibitisha uhusiano wake wa kibinafsi na Afrika, akisema,"Afrika siku zote imekuwa na nafasi ya kipekee moyoni mwangu. Kila mwanamke niliyemfahamu katika ziara zangu barani Afrika alinionesha sura tofauti ya uvumilivu, imani na mshikamano.”

Akiangazia mipango muhimu, alitaja Soko la Sanaa za Mikono la Afrika na Nyumba ya Utamaduni, iliyoanzishwa kusaidia ushiriki wa wanawake wa Kiafrika kiuchumi. “Ninaamini kuwa jukwaa hili litaleta suluhisho madhubuti na endelevu kwa changamoto zinazowakumba wanawake katika juhudi zao za ujasiriamali."

Jukwaa hilo linaendelea kutumika kama nafasi ya kuimarisha uhusiano wa Uturuki-Afrika kwa kuzingatia kuwawezesha wanawake kama mawakala muhimu wa mabadiliko na maendeleo.

InayohusianaTRT Afrika - Istanbul kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Uturuki na Afrika la Biashara na Uchumi 2025

CHANZO:TRT Afrika