UTURUKI
2 dk kusoma
Rais Erdogan aupongeza uungwaji mkono wa Afrika Kusini kwa ajili ya Palestina
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Paul Mashatile, walikutana jijini Ankara kujadili masuala ya kikanda na kimataifa.
Rais Erdogan aupongeza uungwaji mkono wa Afrika Kusini kwa ajili ya Palestina
Erdogan aliitakia Afrika Kusini mafanikio katika maandalizi yake ya mkutano wa G20 utakaofanyika mwezi Novemba. /
15 Oktoba 2025

Rais Erdogan alimweleza Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Paul Mashatile, kwamba Uturuki inashukuru uungaji mkono wa Afrika Kusini kwa ajili ya Palestina wakati walipokutana Ankara.

Mkutano huo ulifanyika katika Ikulu ya Rais na ulijumuisha mazungumzo kuhusu uhusiano wa mataifa hayo mawili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa, kulingana na taarifa kutoka Idara ya Mawasiliano ya Uturuki iliyotolewa kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki, NSosyal.

Erdogan alimweleza Mashatile kuwa Ankara inafuatilia kwa makini usambazaji wa misaada ya kibinadamu usiyokatizwa kwa Gaza na utekelezaji wa kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel.

Erdogan pia aliitakia Afrika Kusini mafanikio katika maandalizi yake ya mkutano wa G20 utakaofanyika mwezi Novemba, na kusema ya kwamkuwa Uturuki itawakilishwa kwenye mkutano huo kwa njia bora zaidi.

Rais huyo wa Uturuki alisema wanajitahidi kukuza ushirikiano kati ya mataifa haya mawili na kuelezea matumaini yake kuwa maamuzi yaliyofikiwa na nyaraka zilizotiwa saini wakati wa mkutano wa kwanza wa Tume ya Kitaifa ya Pande Mbili yatakuwa na mafanikio mazuri.

Mnamo Desemba 2023, Afrika Kusini ilianzisha kesi kubwa dhidi ya Israel katika Mahakama ya Haki za Kimataifa (ICJ), ikidai ukiukwaji wa Mkataba wa Uhalifu wa Mauaji ya Halaiki wa mwaka 1948 katika vita vya Gaza, vita vilivyozimwa baada ya tangazo la kusitisha mapigano lililotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump mwanzoni mwa mwezi huu.

Kati ya Januari na Mei 2024, ICJ ilitoa maagizo ya muda yaliyomlazimu Israel kusitisha mauaji ya halaiki, kusitisha operesheni zake za kijeshi, na kuruhusu upatikanaji wa msaada wa kibinadamu katika ukanda huo.

CHANZO:AA