UTURUKI
2 dk kusoma
Kongamano la 'Zero Waste' laanza Istanbul kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu
Mke wa Rais wa Uturuki, Emine Erdogan, ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu Mradi wa Kutokuwepo kwa Taka 'Zero Waste;, anatarajiwa kuhutubia kongamano hilo.
Kongamano la 'Zero Waste' laanza Istanbul kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu
Jukwaa la 'Zero Waste' laanza mjini Istanbul. /
tokea masaa 16

Kongamano la Kutokuwepo kwa Taka limeanza siku ya Ijumaa mjini Istanbul, likiandaliwa na Taasisi ya ‘Zero Waste’, iliyoanzishwa chini ya uangalizi wa mke wa Rais wa Uturuki, Emine Erdogan, kwa kushirikiana na Wizara ya Mazingira, Miji na Mabadiliko ya Tabianchi, pamoja na Wizara ya Kilimo na Misitu.

Mradi wa ‘Zero Waste’ ulianzishwa na Emine Erdogan, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu ‘Zero Waste’ na pia Mwenyekiti wa heshima wa taasisi hiyo, kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa.

Kongamano hili linafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, chini ya kaulimbiu: "Watu, Maeneo, Maendeleo".

Mada kuu zitakazojadiliwa ni pamoja na kubadilisha sera kuwa vitendo, kupanua wigo wa suluhu, kuhamasisha ufadhili, na kujenga ushirikiano.

Wakati wa kongamano hilo la siku tatu, ambalo linahudhuriwa na washiriki kutoka nchi 104 na wadau wa kimataifa 118, vikao vya mijadala vitagusia mada kama vile maana ya "zero waste" (kutokuwa na taka kabisa), kanuni na sheria, fedha, taka za kikaboni, mustakabali wa mitindo ya mavazi, uchakataji, athari za akili mnemba (AI), teknolojia, na suluhisho mbalimbali.

Miongoni mwa wageni waalikwa ni Guy Bernard Ryder, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na sera, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres; Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat, Anaclaudia Rossbach; pamoja na Mwakilishi Maalum wa Rais wa Azerbaijan kwa masuala ya tabianchi, Mukhtar Babayev.

Kongamano hilo pia linahudhuriwa na Waziri wa Mazingira wa Uturuki, Murat Kurum, pamoja na Waziri wa Kilimo na Misitu, Ibrahim Yumaklı, na linatarajiwa kufungwa siku ya Jumapili.

Taasisi ya ‘Zero Waste’ ilianzishwa mwaka 2023 chini ya uangalizi wa mke wa rais. Taasisi hiyo inalenga kukuza Mradi wa ‘Zero Waste’ na kuhakikisha unaendelea kwa kudumu.

Tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Bodi ya Ushauri ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ‘Zero Waste’, pamoja na sekretarieti ya ‘Zero Waste’ inayojumuisha UN-Habitat na UNEP.

CHANZO:AA