UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan asisitiza uungaji mkono wa Uturuki kwa azimio la Sharm el-Sheikh la Gaza
Erdogan, Trump, Sisi na Al Thani walitia saini rasmi makubaliano ya kuunga mkono mapatano na amani ya kudumu huko Gaza.
Erdogan asisitiza uungaji mkono wa Uturuki kwa azimio la Sharm el-Sheikh la Gaza
Uturuki itaunga mkono kikamilifu azimio la Sharm el-Sheikh. / / AA
15 Oktoba 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amethibitisha uungaji mkoni wa Uturuki kwa azimio la Mkutano wa Amani wa Sharm el-Sheikh wa Gaza iliyotiwa saini wiki hii.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa baraza la mawaziri jijini Ankara siku ya Jumatano, Erdogan alisema, "Tutaunga mkono kikamilifu azimio la Sharm el-Sheikh hadi mwisho, na ninaamini Marekani, Misri na Qatar zitakua na msimamo kama huo."

Matamshi hayo yanafuatia mkutano wa kilele wa siku ya Jumatatu katika mji wa Sharm el-Sheikh nchini Misri, ambapo Rais Donald Trump wa Marekani na Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi waliwakaribisha viongozi zaidi ya 20 wa dunia akiwemo Erdogan kutia saini hati kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza yaliyomaliza vita.

Erdogan, Trump, Sisi na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani walitia saini rasmi makubaliano ya kuunga mkono mapatano na amani ya kudumu huko Gaza.

Kuhusu hali ya kibinadamu huko Gaza, Erdogan alisisitiza umuhimu wa juhudi za kimataifa kuwasaidia Wapalestina.

"Kila jitihada za kupunguza shida za watu wanaodhulumiwa wa Gaza ni wa thamani kwetu. Si mahali pa mtu yeyote wala hakuna mtu mwenye haki kudharau hili kwa kusema, 'walitia tu saini usitishaji vita,'" alisema.

Kuachiliwa kwa Wapalestina waliokuwa wamefungwa katika jela za Israel kulianza baada ya Hamas kuwaachilia huru wafungwa wote 20 wa Israel waliokuwa wameshikiliwa huko Gaza siku ya Jumatatu.

Erdogan pia aliangazia jukumu la Uturuki katika kukuza uthabiti wa kikanda, akisema: "Watu wa Uturuki wamefaulu mtihani wa udugu na ujirani. Uhusiano wetu na Syria unaimarika. Uthabiti unapokita mizizi nchini Syria, kila kitu kitaboreka kwa kiasi kikubwa."

CHANZO:TRT World