Makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza ni hatua muhimu kuelekea kuleta amani ya kudumu katika eneo hilo, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya Uturuki imesema.
"Tunatumai kwamba hatua hii itakuwa mwanzo wa amani ya kina, ya haki, na endelevu na hatimaye itachangia katika lengo la suluhu la mataifa mawili," msemaji wa wizara hiyo Zeki Akturk aliambia mkutano na waandishi wa habari wa kila wiki jijini Ankara siku ya Alhamisi.
Kando na hilo, katika kujibu swali kuhusu ushiriki wa Uturuki katika kikosi kazi cha Gaza, vyanzo vya wizara vilisema kwamba "kwa uzoefu tulionao kutoka kwa misheni ya amani ya hapo awali, Vikosi vya Wanajeshi wa Uturuki viko tayari kufanya kazi yoyote iliyopewa ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa za uanzishaji na kudumisha amani na kazi inafanywa kwa uratibu na taasisi za serikali."
Uturuki inaunga msimano wa 'nchi moja, jeshi moja' nchini Syria
Kuhusu kundi la kigaidi la SDF kujumuishwa katika jeshi la Syria, duru za habari zilisema "serikali ya Syria inaendelea na juhudi zake za kufanyia marekebisho taasisi na vyombo vyake vyote, pamoja na kuweka utulivu na usalama nchini humo.
Katika muktadha huu, tunaendelea na juhudi zetu za kuimarisha uratibu na ushirikiano na Wizara ya Ulinzi ya Syria, kwa lengo la kuimarisha uwezo wa usalama wa Syria na kuchangia kuanzishwa kwa utulivu na usalama katika eneo hilo kwa kuondoa ugaidi.
"Sambamba na utulivu na usalama wa Syria, tunasalia na nia ya kuunga mkono msimamo wa serikali moja na jeshi moja. Katika suala hili, kujumuishwa kwa kundi la kigaidi la SDF katika jeshi la Syria ni muhimu sana. Kama Uturuki, tunafanya uratibu unaohitajika na wenzetu juu ya suala hili na tunafuatilia kwa karibu mchakato huo," vyanzo viliongeza.